SERIKALI YAONYA WAKURUGENZI KUKAIMISHA WAKUU WA IDARA
Na Antony Sollo Biharamulo.
Serikali imetoa onyo kali kwa Wakurugenzi wa
Halmashauri nchini
kutokaimisha wakuu wa Idara kwa zaidi ya miezi sita
na kuonya kuwa Mkurugenzi atakayekaidi agizo hilo atachukuliwa
hatua kali.
Akizungumza na Watumishi wa Halmashauri ya Wilaya ya
Biharamulo Mkoani Kagera Naibu Waziri wa Nchi Ofisi ya Rais
Menejimenti Utumishi wa Umma na Utawala Bora Bi Mary Mwanjelwa amewataka
Wakurugenzi wa Halmashauri nchini
kutokaimisha nafasi katika idara
mbalimbali kwa zaidi ya miezi sita
vinginevyo hatua kali zitachukuliwa
kwa atakayekaidi agizo hilo.
Bi Mwanjelwa alisema kuwa Serikali imeshatoa waraka
kwa Wakurugenzi nchini juu ya agizo la kutomkaimisha ukuu wa idara kwa kipindi cha zaidi ya miezi sita bila kupandishwa daraja kushika nafasi hiyo vinginvyo
Mkurugenzi anapaswa kujieleza
kabla ya kuwajibishwa kwa kushindwa kutii agizo la serikali.
Serikali
imeshatoa waraka kwa Wakurugenzi
nchini juu ya agizo la kutomkaimisha ukuu wa idara kwa kipindi cha zaidi ya miezi sita bila kupandishwa daraja kushika nafasi hiyo vinginvyo Mkurugenzi anapaswa kujieleza kabla ya kuwajibishwa kwa kushindwa kutii agizo la serikali “Serikali ilishatoa waraka kwa Wakurugenzi wa Halmashauri nchini juu ya agizo la kutomkaimisha ukuu wa idara kwa kipindi cha zaidi ya miezi sita bila
kupandishwa daraja kushika nafasi hiyo vinginvyo Mkurugenzi atapaswa kujieleza kabla ya kuwajibishwa kwa kushindwa kutii agizo la serikali”alisema Mwanjelwa.
Kwa upande wake Mkurugenzi wa Halmashauri ya Wilaya
ya Biharamulo Bi Wende
Ng`ahala alisema agizo hilo
limeshaanza kutekelezwa baada ya kukaa kikao Maalumu cha baraza la Madiwani hivi karibuni
kwa lengo la kupitisha wakuu wa idara walio na sifa za kuwa
wakuu wa idara kamili.
“Agizo hilo limeshaanza kutekelezwa baada ya kukaa kikao Maalumu cha baraza la Madiwani
hivi karibuni kwa lengo la
kupitisha wakuu wa idara walio na sifa za kuwa wakuu wa idara
kamili”alisema Ng`ahala.
Bi Mwanjelwa anaendelea na ziara yake Mkoani Kagera
kwa kukagua shughuli mbalimbali zinazofanywa na TASAF Wilayani
humo ambapo alitembelea makundi ya walengwa katika Kata za
Katoke na Lusahunga ili kujionea namna ambavyo wananchi wamenufaika na fedha
hizo.
Akitoa taarifa kwa Naibu waziri Mratibu wa TASAF
Wilaya ya Biharamulo Bwana Wanna
Nyagarogoro alisema zaidi ya
Shilingi mil 66,833,72 zimetumika katika Mpango wa kunusulu kaya maskini
katika Kata ya Nyarubungo Kijiji cha Katoke huku Kata ya Lusahunga
ikitumia zaidi ya Sh Mil 160,962,813.65 na kuongeza kuwa fedha hizo
zimeleta mabadiliko chanya kwenye jamii katika kuboresha huduma za
Elimu,mavazi,chakula na Bima ya Afya.
Bi Mwanjelwa alisema kuwa katika kuboresha huduma na
kudhibiti fedha hizo Serikali ina mpango wa kuwaingizia walengwa wa
mpango huo fedha kwa njia ya MPESA na kuwataka wataalamu kuwaongoza
walengwa kufanya kazi zenye ubora ili kuwa na matokeo chanya pia
serikali inatarajia kuanza mchakato wa kuingiza walengwa wapya ili
kuhakikisha wale ambao hawakuhaulisha kutokana na vijiji vyao kutokuingizwa
katikam mpango huo waweze
kunufaika na mpango huo.
MWISHO
No comments: