MAKALA KUHUSU MAENDELEO YA SEKTA YA KILIMO
Mapuli Simon Lukanya : Mkulima anayetarajia
Makubwa kupitia Sekta
ya kilimo.
Na Antony Sollo
Hii
ni Makala Maalumu iliyoandaliwa na Mwandishi wa Habari wa gazeti la Tanzania
Daima na Mapuli Simon Lukanya Mkulima na mkazi wa Kijiji cha Sanjo Kata ya
Usagara Wil.aya ya Misungwi Mkoani Mwanza.
Tanzania
Daima ilitembelea shambani kwa mkulima huyo ili kujionea namna Mapuli alivyo na
ndoto ya kuwa mkulima mkubwa wa mazao mbalimbali ikiwemo ufugaji wa Nyuki ambapo
baada ya kufika katika maeneo ya mkulima huyo yaliyoko katika kitongoji cha
Isasabudaga alikutana na Shamba kubwa la mpunga lenye ukubwa wa ekari sita
ambazo zimepandwa mpunga,huku ekari tatu zikiwa ni maalumu kwa ajili ya kilimo
cha bustani.
Tanzania
Daima pia imepata fursa ya kuona shamba lenye ukubwa wa ekari thelathini ambapo
katika shamba hilo imepandwa miti aina ya mikaritusi kwa ajili ya utunzaji wa
mazingira ambapo miti hiyo itatoa miti aina ya mirunda kwa ajili ya shughuli za
ujenzi.
Katika
hatua nyingine Mapuli amelieleza Tanzania Daima kuwa,pamoja na kuwa na maeneo
yenye ukubwa wa ekari zipatazo arobani ni ekari saba tu ambazo zilipatikana na
kufanikiwa kupanda zao la muhogo kwa ajili ya matumizi ya chakula na biashara.
Akizungumza
na Tanzania Daima Mapuli alianza kwa kusema.
Mimi
kwa jina naitwa Mapuli Simon Lukanya,ni mkaazi wa Kijiji cha Sanjo Kata ya
Usagara Wil.aya ya Misungwi Mkoani Mwanza ni mkulima mdogo ambaye nina ndoto ya
kupata mafaniki makubwa kutokana na Sekta ya Kilimo.
Nilianza
kujishughulisha na shughuli za kilimo nikiwa na ndoto ya kuwa mkulima mkubwa
ambapo hadi sasa nimejiendeleza mwenyewe bila msaada wowote toka katika taasisi
yoyote ya binafsi au Serikali.
Changamoto.
Kuhusu
changamoto anazokumbana nazo Mapuli anasema, moja ya changamoto anazoona kuwa
ni kikwazo cha maendeleo yake ni pamoja na Mtaji,zana za kilimo,pamoja na
ushauri wa kitaalamu toka kwa wataalamu wa Sekta ya Kilimo pamoja na Mvua.
Katika
hatua nyingine Mapuli amewaomba wadau wa maendeleo ikiwemo Serikali pamoja na
taasisi binafsi kusaidia namna ya kumpatia Elimu juu ya ukulima wa kisasa
pamoja na kumpatia mafunzo ili kukuza uelewa juu ya matumizi mbalimbali ya zana
za kilimo pamoja na mabadiliko ya tabia nchi.
Mapuli
amewaomba wadau mbalimbali wa masuala ya kilimo ndani na nje ya nchi wajitokeze
kwa ajili ya kumpa ushirikiano wa karibu katika masuala ya kifedha,ushauri wa
kitaalamu pamoja na uwezeshaji ili aweze kutimiza ndoto yake
Mapuli
Simon Lukanya akiwa shambani kwake maeneo ya Sanjo Kata ya Usagara Wilaya ya
Misungwi Mkoani Mwanza. Picha na Antony
Sollo
Mapuli
Simon Lukanya akifurahia jinsi mwaka huu unavyoonyesha matumaini kwake baada ya
kulima mara kadhaa na kukwamishwa na mvua kama alivyoeleza kuwa moja ya
changamoto kubwa kwake ni pamoja na mvua kushindwa kunyesha jambo analoona ni
kikwazo kikubwa cha mafanikio yake.Picha
na Antony Sollo
No comments: