UTPC YAWATAKA WAANDISHI KUACHA MIGOGORO
Mkurugenzi Mtendaji wa Shirikisho la Vilabu vya Waandishi wa Habari
Nchini (UTPC), Bw Abubakar Karsan akiwa na Waandishi wa Habari Mkoani Geita
|
Na Antony Sollo Geita.
Mkurugenzi Mtendaji wa Shirikisho la Vilabu vya Waandishi wa Habari
Nchini (UTPC),Bw Abubakar Karsan amewataka Waandishi wa Habari Mkoani
Geita kuachana na Migogoro ambayo imekuwa ni chanzo cha kukwamisha
maendeleo ya Klabu hiyo ,huku akiwataka kutumia kalamu yao kuandika
Habari kuhusiana na fursa zilizopo Mkoani humo.
Karsani ametoa kauli hiyo wakati akifungua Mkutano Mkuu wa dharura
ulioitishwa kwa ajili ya kuchagua viongozi wa muda watakaoiongoza
Klabu ya Waandishi wa Habari ya Mkoa wa
Geita kwa kipindi cha
mwaka mmoja baada ya uongozi uliokuwepo
hapo mwanzo
kutenguliwa na wananchama wa chama chama hicho.
Awali Bw.Karsan aliwataka Waandishi wa Habari Mkoani humo kuhakikisha
wanaipa nguvu Sera ya Viwanda kwa kuandika na kutangaza fursa ambazo
zinapatikana.
“Ndugu Waandishi wa Habari wa Mkoa huu naomba kuwaambia ninyi ni Klabu
muhimu mno maana Mkoa huu ndiyo anakotoka Rais wa Jamhuri ya Muungano
wa Tanzania ni aibu kuendekeza migogoro isiyo natija kwa maendeleo ya
Tasnia ya Habari nawaomba mchague Viongozi wasafi wasio
walafi,wabinafsi maana kufanya hivyo kutawarudisha nyuma
kimaendeleo”alisema Karsan.
Aidha Bw.Karsan aliwaomba waandishi wa Habari wa Klabu hiyo mara
watakapoitisha Mkutano Mkuu wa 2020 wamuombe Rais wa Jamhuri ya
Muungano wa Tanzania Dkt John Pombe Magufuli kuwa Mgeni Rasmi.
“Ninyi ni Klabu ambayo ni sawa na Kioo maana Mkoa wenu umefanikiwa
kutoa Kiongozi Mkuu wa Nchi hivyo nawaomba Mkafungue Tawi Wilaya ya
Chato na mjitahidi kuandika Habari za kuutangaza Mkoa wa Geita pamoja
na Historia ya Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania”alisema Karsan.
Katika Uchaguzi huo aliyechaguliwa kishika nafasi ya Mwenyekiti ni
Mutta Robart ,Makamu Mwenyekiti wake akiwa ni Esther Sumira,Katibu
Mkuu Mtendani wa Klabu hiyo ni Emmanuel Ibrahimu,huku nafasi ya Katibu
Msaidizi akishikiliwa na Joel Maduka,nafasi ya Mweka hazina
imeshikiliwa na Editha Edward ,na Msaidizi wake Anna Ruhasha, kwa
upande wa wajumbe wa Kamati Tendaji ni Renatus Masuguliko,Antony
Sollo na Alphonce Kabilando.
Wakizungumza baada ya Uchaguzi huo Wanachama wa klabu hiyo wameomba
Viongozi kuwa wawazi kwenye shughuli za kila siku na kuachana na mambo
ya usiri na ubinafsi.
Mwenyekiti mpya wa Klabu hiyo Mutta Robart aliwashukuru wanachama wa
Klabu hiyo kwa kumuuamini kushika wadhifa huo ambapo aliwaahidi kuwapa
ushirikiano na kusema kuwa nafasi waliyompa ataitendea Haki na kwa
kufuata Katiba.
“Nawashukuruni sana kwa kuniamini na kunikabidhi jukumu hili la
kuongoza Chama hiki nawaahidi nitaitendea Haki nafasi hii na pia
nitafuata Katiba maana ndiyo kiongozi wetu”alisema Mutta.
MWISHO
No comments: