RC GABRIEL FEDHA ZA UMMA ZIKO SALAMA
Na Antony Sollo Geita
MKUU wa mkoa wa Geita Mhandisi
Robert Gabriel amesema kuwa fedha zinazotolewa na Serikali kwa sasa ziko salama
na kusisitiza kuwa biashara ya upigaji dili kwa fedha za umma, ubabaishaji kwa
sasa havina nafasi katika mkoa wake na kwamba Geita ni mkoa salama kwa fedha za
umma
Mkuu Huyo wa Mkoa ameyasema hayo
jana mjini Geita wakati akimkaribisha Waziri wa Habari, Sanaa, Utamaduni na
Michezo Dk Harrison Mwakyembe wakati alipokuwa akitoa taarifa ya maendeleo ya
mkoa kuhusiana na sahughuli mbalimbali za maendeleo ya mkoa na uwekezaji
Gabriel alisema kabla hajahamishiwa
mkoani Geita akitokea mkoani Tanga, aliikuta Geita ikiwa imesheheni wapiga dili
na watu wanaotumia fedha za umma vibaya na kuonya kuwa kwa sasa watumishi wa
aina hiyo hawana nafasi kwenye uongozi wake
Akitolea mfano wa matumizi mabaya
ya fedha za umma, alisema kuanzia mwaka huu alibaini kiasi cha fedha Sh bilioni 55 zikiwa
zimetumika vibaya katika ujenzi wa vyumba vya madarasa vya shule ya msingi
Nyakumbu majengo ambayo hayaendani na fedha zilizotumika
Mhandisi Gabriel alisema “ Mimi
nashangaa watu wa Mungu wanomba makanisani Mungu atupe utajiri, wakati tayari
Mungu alishatoa utajiri kwa watu wa mkoa wa Geita, sasa niwashauri waombe Mungu
ili kukamata wezi na mafisadi Geita”,
Aliongeza kuwa mkoa wa Geita ni
mkoa uliobarikiwa na kuomba kuwa
takwimu za kiuchumi zinazotolewa kuhusu uchumi wa mikoa mbalimbali
kitaifa na kimataifa zinatakiwa zipitiwe upya ili kutoa hali halisi kwamba
Geita ndiyo mkoa unaoongoza kwa kuzalisha dhahabu kwa wingi kuliko mkoa wowote
hapa nchini
Mhandisi huyo alisema kuwa kwa
ushirikiano wa Serikali na Kampuni ya magazeti ya Serikali (TSN) wamebaini kuwa
mkoa wa Geita una fursa nyingi za kiuchumi ambazo zilikuwa hazijawekwa bayana
kwa umma na wawekezaji wa ndani na nje , hivyo kuwaomba wandishi wa habari
kumpatia ushirikiano kwa kutangaza fursa za kiuchumi zilizopo kwa manufaa
mapana ya maendeleo ya mkoa na taifa kwa ujumla
Naye Naibu Katibu Mkuu Wizara ya
Elimu Dk Avemaria Semakafu alisema kuwa
amefarijika na mabadiliko ya utendaji yalyofanywa na Mkuu wa Mkoa wa Geita
Mhandisi Gabriel na kushauri Chuo cha Veta kinachojengwa mkoani Geita kichikite
katika kutoa taaluma inayohusu uchimbaji, uchakataji wa raslimali zilizo katika
mkoa wa Geita hasa madini, samaki na asali
Kwa upande wake Msemaji Mkuu wa
Serikali Dk Hassan Abbas alisema kuwa kitengo chake kitaunga mkono kwa dhati
juhudi znazofanywa na Mkuu wa mkoa wa Geita katika kuwaletea wananchi maendeleo
ili zifahamike vyema kwa umma na kuifanya Geita kuwa kitovu cha dhahabu nchini
Dk Abbas alisema katika kufanikisha
azma hiyo, .atatuma timu tatu za wandish.i wa habari kutoka TBC,.Idara ya
Habari Maelezo na .Kampuni ya magazeti
ya serikali kwa madai kuwa teknolojia kwa sasa imebadilika hivyo ni vyema
kutumia teknojia ya habari kutoka kwenye vyombo hivyo vya umma.
“ Mimi Mkuu wa mkoa nitakuunga
mkono kwa kukuletea timu tatu, ya anga, majini na nchi kutoka kwenye vyombo vya
serikali, nikimaanisha anga ni TBC, majini ni Idara ya Habari Maelezo na Nchi
kavu ni vyombo vya magazeti ya umma –TSN”, alisema.
Kwa upande wake Waziri wa Habari,
Sanaa, Utamaduni na Michezo Dk Harrison Mwakyembe alimpongeza Mkuu wa Mkoa wa
Geita kwa utendaji kazi uliotukuka na kuuomba uongozi wa TSN kuendelea
kuwaruhusu wandishi wa habari kutoa ushirikiano kwa serikali kuendelea kuandika
na kutangaza habari za ukweli juu ya fursa za kichumi zilizopo mkoani Geita.
“ Taarifa hii uliyoitoa leo Mkuu wa
mkoa ni ya aina yake, nimetembea mikoa mingi lakini sijawahi kuona uwasilishaji
wa taarifa ya namna, ni taarifa iliyosheheni weledi mkubwa isiyotiliwa shaka na
inayoaminika, hongera sana”, alisema Dk Mwakyembe
Kuhusu kusitishwa kwa chaneli za
umma zlizokuwa zinarusha matangazo yake kupitia visumbusi vya Azama, DSTV na
Zuku alisema kuwa kuna upotoshaji kwa umma unaosambazwa kupitia mitandao ya
kijamii kwamba serikali haitaki wananchi wake wapate taarifa kupitia visumbusi hivyo,
jambo ambalo alisema halina ukweli wowote.
“ Ukweli ni kwamba, vyombo hivyo
vilikiuka sheria ya kurusha matangazo kinyume na usajili, na sisi kama serikali
tulikuwa hatujazungumzia jambo kwakuwa wamiliki wa visumbusi hivyo walipeleka
shauri mahakamani, na kwakuwa sasa tumeshinda tumechukua hatua stahiki ya
kuzuia wizi kwani, walipaswa kuonyesha taarifa zao bure na sio kuwaibia
wananchi kama walivyokuwa wanafanya”, alisema
MWISHO
No comments: