Aaron Ramsey alishinda magoli 2 na kuiwezesha timu yake kuinyoa Sunderland 3-1 huku meneja Paolo Di Canio akipewa kadi nyekundu
Arsenal watamba
Goli la kwanza lilipatikana baada ya kuhudi za mchezaji mpya aliyesajiliwa na Arsenal Mesut Ozil ambaye alimwandalia pasi murua Olivier Giroud aliyenusa nyavu.
Goli hilo lakini lilisawazishwa na Craig Gardner muda mfupi baada ya mapumziko.

Magoli
mengine mawili ya Arsenal yalitiwa kimiani na Ramsey na kuiwezesha timu
yake kuandikisha ushindi wa mabao 3-1 ambao ni wa tano mfululizo.
Manchester City yapoteza mwelekeo.
katika mechi nyingine,Stoke City itajilaumu
yenyewe kwa kupoteza nafasi kadhaa murua za kuishinda Manchester City
katika mechi ambayo ilimalizika kwa matokeo ya 0-0
Manchester City ilitawala kipindi cha kwanza kwa
kumiliki mpira lakini mara kwa mara wakashindwa kuvunja ngome ya Stoke
ambao bado wanaendelea kufanya vyema katika tangu ligi ilipoanza.
Matokeo haya hayamsaidii lolote meneja mpya wa
Manchester City kwa kuwa bado anahangaika kuisuka timu hiyo na
haijacheza kwa kiwango chake.
No comments: