Taasisi yaTiba ya Mifupa na Mishipa ya Fahamu (MOI) imepanga kutumia zaidi ya Bilioni 17 katika ujenzi wa awamu ya Tatu ya Mradi wa Taasisi yaTiba ya Mifupa na Mishipa ya Fahamu (MOI phase 111)
Meneja Uhusiano wa Taasisi
ya Tiba ya Mifupa na Mishipa ya Fahamu (MOI) Bw. Jumaa Almasi akionesha kwa
waandishi wa Habari (hawapo pichani) Picha ya sehemu ya kichwa iliyowekewa
kifaa maalum(Mayfield Clamp). kulia ni Afisa Uhusiano wa Taasisi hiyo Bw.
Patrick Mvungi
Meneja
Uhusiano wa Taasisi ya Tiba ya Mifupa na Mishipa ya Fahamu (MOI) Bw. Jumaa
Almasi akieleza kwa waandishi wa Habari (hawapo pichani) Mipango mbalimbali
ya Taasisi hiyo ikiwamo utekelezaji wa awamu ya tatu ya MOI (MOI Phase III)
itakayosaidia kuboresha huduma za afya nchini,kulia ni Afisa Uhusiano wa
Taasisi hiyo Bw. Patrick Mvungi na kushoto ni Afisa Habari wa Idara ya
Habari(MAELEZO) Bw. Frank Mvungi.
Taasisi yaTiba ya Mifupa na Mishipa ya
Fahamu (MOI) imepanga kutumia zaidi ya Bilioni 17 katika ujenzi wa awamu ya
Tatu ya Mradi wa Taasisi yaTiba ya Mifupa na Mishipa ya Fahamu (MOI
phase 111) hadi mradi huo utakapokamilika mapema mwakani.
Hayo yamesemwa leo na Meneja Uhusiano wa
Taasisi hiyo Bw. Jumaa Almasi wakati akizungumza na waandishi wa habari leo
jijini Dar es salaam.
Almasi alisema kuwa Ujenzi wa jengo hilo
jipya lenye ghorofa 7 ambao unaendelea ukikamilika utaongeza maeneo ya kutolea
huduma,Vitanda vitafikia 380 kutoka 159 vilivyopo sasa hali ambayo itapanua
wigo wa huduma zinazotolewa kwa sasa.
“Mradi huu utasaidia kuongeza ufanisi na
huduma zinazotolewa na taasisi kwani ukikamilika utaongeza maeneo ya kutolea
huduma kwa kupunguza msongamano wa wagonjwa mawodini
kutokana na kuongezeka kwa vitanda kutoka 159 hadi kufikia 380” Alisema Almasi.
Aliongeza kuwa huduma nyingine
zitakazotolewa ni CT SCAN,MRI,huduma za Cybernife na Digital Antiograph
ambazo kwa Sasa hazitolewi katika Taasi hiyo .
Alibainisha kuwa MOI ni moja ya
Taasisi zenye vifaa bora vya upasuaji pamoja na vyumba vya upasuaji
vinavyokikidhi viwango vya kimataifa kusini mwa jangwa la Sahara baada ya
Afrika ya kusini.
Alisema kuwa hali hiyo ni matokeo ya
juhudi kubwa zinazofanywa na Serikali katika kuboresha huduma za afya nchini
ambapo wameweza kupatiwa vifaa vya kisasa pamoja na wataalamu waliobobea
katika huduma za tiba ya mishipa ya fahamu na upasuaji wa uti wa mgongo.
MOI imeendelea kushirikiana na Taasisi za
Kimataifa zinazotoa huduma za afya kama SIGN GROUP ya nchini
Marekani ambayo imekuwa ikitoa msaada wa vifaa tiba ikiwa ni alama ya
ushirikano mzuri uliopo kati ya Taasisi hiyo na mashirika ya Kimataifa.
No comments: