Wanachama 85 waliokuwa CUF, ADC na CCM wilayani Pangani wamehamia CHADEMA
katibu wa kanda ya kaskazini Bw Amani Golugwa akikabidhi bendera na kadi kwa wanachama wapya wa Chadema
Wanachama
85 waliokuwa CUF, ADC na CCM wilayani Pangani wamehamia CHADEMA juzi
mara baada ya kukutana na katibu wa kanda ya kaskazini Bw Amani Golugwa
alipo kuwa anafanya ziara ya kukagua zoezi la Chadema ni msingi wilayani
humo.
Miongoni mwa wamachama hao alielezea namna walivyo wahi kupelekwa kisiwani Pemba wakiwa wamevalishwa mavazi ya kijeshi ili wakapigie kura chama tawala wakati wa uchaguzi wa mwaka 2010.
Zoezi la chadema ni msingi linaendelea kwa kasi mkoani Tanga huku mamia ya wananchi wakizidi kujiunga na chadema, miongoni mwa wananchi hao amekemea propaganda mbaya za udini zilizokuwa zinatumiwa na ccm dhidi ya vyama vya upinzani kwa kusema kuwa zimechangia kwa kiasi kikubwa sana kuleta mgawanyiko na malumbano ya udini yasiyo kuwa na tija kwa taifa.

Alisema mara zote ccm wamewaaminisha watu wa Pangani kuwa CUF ni chama cha waislamu na chadema ni chama cha wakristo lakini hakuna hata siku moja ambayo ccm wamesha wahi kusema kuwa wao ni chama cha watu gani. "...Baada ya sisi kutumiwa sasa tumeamua kufuata chama chenye dhamira na nia ya dhati kutukomboa"
Jana wanachama zaidi ya 70 wa kata ya kiomoni wilayani Tanga ambayo hivi karibuni kwenye uchaguzi wa kitongoji chadema iliibuka mshindi wamejiunga na chadema na wako kwenye maandalizi ya kushinda kiti cha udiwani kilicho wazi kwenye uchaguzi mdogo unao tarajiwa kufanyika mapema mwezi Februari.
No comments: