Mashirika ya kutoa misaada yamesema kuwa maelfu ya watu wamelazimika kuhama makwao kufuatia mapigano nchini Sudan Kusini na wanahitaji misaada ya dharura
Wengi wamekimbia kambi moja iliyoko ufuko wa mto nile, baada ya
kuvuka mto huo kwa mashaua ili kuepuka mapigano yanayoendelea mjini Bor
kati ya wafuasi wa rais Salva Kirr na aliyekuwa naibu wake Riek Machar.
Mwandishi wa BBC, mjini humo amesema kuwa wakimbizi hao wamepiga kambi chini ya miti wakiwa na mali yao waliyofanikiwa kubeba.
Afisa mkuu wa Shirika la madaktari wasiokuwa na
mipaka Medicins san Frontiers, MSF limesema hakuna maji masafi ya
kunywa. Amesema watu wanakunywa maji chafu ya mto nile.
Amesema watu wengi wanajisaidia hadharani
kutokana na ukosefu wa vyoo na hivyo kuongeza tishio la kuzuka kwa
ugonjwa wa kuraha na kutapika
Habari na BBCswahili.com
Habari na BBCswahili.com
No comments: