Mazungumzo ya kupatanisha pande mbili zinazozozana kwenye mgogoro wa Sudan Kusini na kusitisha vita, yameanza mjini Addis Ababa Ethiopia
Kwa mujibu wa taarifa kutoka katika wizara ya mambo ya nje nchini
Ethiopia, wajumbe kutoka kanda ya Afrika Mashariki wananuia kusuluhisha
mgogoro huo wa kisiasa ambao umekuwa ukitokota kwa takriban wiki tatu.
Hata hivyo mazungumzo ya ana kwa ana yangali kuanza kati ya pande zinazozozana yangali kuanza.
Wawakilishi kutoka pande zinazozozana wanakutana
na wajumbe wa kikanda wanaoendesha mazungumzo hayo ingawa haijulikani
ikiwa viongozi wa Sudan Kusini wenyewe watakutana ana kwa ana.
Mamia ya maelfu ya raia wa nchi hiyo wameachwa
bila makazi kufuatia mapigano hayo kati ya majeshi ya Rais Salva Kiir na
yale ya hasimu wake ambaye alikuwa makamu wake wa Rais Riek Machar
Wakati huo huo, ubalozi wa Marekani, katika mji
mkuu wa Sudan Kusini,Juba unaendelea na shughuli ya kuwahamisha
wafanyakazi wake wote nchini humo kutokana na mzozo unaoendelea.
Umoja wa Mataifa umesema kuwa hautarajii raia wa Marekani wanaofanya kazi na shirika lake lolote kuondoka.
Waasi wakiongozwa na makamu wa rais wa zamani Riek Machar wamekuwa wakipambana na wanajeshi wa serikali tangu mwezi uliopita.
Habari na BBCswahili.com
Habari na BBCswahili.com
No comments: