HABARI ZILIZOVUTA HISIA MWAKA 2017 KATIKA MKOA WASHINYANGA
Mbwembwe pamoja na ushangiliaji wa
aina yake zilivyotawala katika Uchaguzi ndani ya Chama cha Mapinduzi Mkoani Shinyanga
kwa mwaka 2017
Wahenga walishasema,ukitaka uhondo wa Ngoma ingia ucheze!!!!!!
Hivi ndivyo ilivyokuwa katika uwanja wa siasa ndani ya CCM
Mkoani Shinyanga ambapo wanachama wa chama hicho walibuni
mbinu ya kuhamasisha namna ya kumpata Mwenyekiti wa Chama hicho Mkoani humo ambapo
ilikuwa ni burudani tosha kwa watazamaji wa Uchaguzi wakiwemo waandishi wa
Habari.
Kabla ya Uchaguzi na hatua ya kutangaza matokeo ya Uchaguzi
ndani ya CCM Mkoani shinyanga kuliibuka mbwembwe na ushangiliaji wa aina yake
ambao hautakaa usahaulike.
Mmoja wanachama wa Chama cha Mapinduzi waliotia fola kwa mwaka
2017 ni Mheshimiwa Diwani wa Kata ya Kiloleli iliyoko Wilaya ya Kishapu Mkoani
Shinyanga Manyama.
Diwani huyo alijizolea
umaarufu baada ya kubuni mbinu ya kupiga kampeni akitumia chupa ya chai
(Thermos) ambayo ilikuwa imetundikwa katikamoja ya nguzo na kila aliyekuwa
akipita aliitikisa na hata kuibusu kama ishara fulani kuonyesha dira na
mwelekeo wa mgombea waliyekuwa wameona ataweza kuivusha CCM katika Uchaguzi
2020.
Mwandishi wa Makala hii alifuatilia nini ilikuwa uhalisia juu ya
chupa ya chai iliyokuwa imetundikwa kama mtindo mpya wa upigaji kampeni ambapo
kupata ufafanuzi huo mwandishi alimtafuta Diwani wa Kata ya Kiloleli ambaye
alikuwa na haya ya kuzungumza.
Mwandishi: Mheshimiwa Diwani naomba kufahamu ni
kipi kilichopelekea mtundike chupa ya chai katika moja ya nguzo za hema
iliyokuwa ndani ya ukumbi wa kupigia kura.
Diwani: ndugu mwandishi,hii ni mbinu mpya
tuliyoibuni baada ya kukutana na kukubaliana namna gani tutaweka ishara kwa
ajili ya kusaidia upigaji wa kampeni kwa mtu wetu ambaye tunaamini anazo sifa
za kuivusha CCM katika chaguzi zijazo ukiwemo wa 2020.
Mwandishi:Mbinu hii imebuniwa na nani?
Diwani: “Mbinu hii nimeiasisi mimi,si unajua
siasa ni ushindani na siasa kwa upande mwingine ni ubunifu? Sisi kama wapiga
kura baada ya kukaa na kuwapima wagombea wetu walioomba kupigiwa kura tuliona
nani atakisaidia chama kukifikisha pale tunapotaka na hasa kwa kuendana na kasi
ya Mheshimiwa Rais yaani HAPA KAZI TU”
Mwandishi: kwa hiyo mlikuwa mnapiga kura mkijua
ni wapi na ni nani anayeshinda?
Diwani: Hapana! Kutokana na mfumo wa Demokrasia,kila
mtu anayo haki ya kuchagua mtu au kiongozi anayemtaka hivyo baada ya kupiga
kampeni nikiwapa wazo langu wanachama kwa ujumla wao,tulikubaliana kuwa kwa
wale watakaokuwa tayari kuniunga mkono juu ya maoni na mawazo yangu ishara kubwa
ni kufika na kuibusu na kuitikisa chupa hiyo na ndiyo kilichotokea na baada ya
kuona watu wengi wakipita na kuibusu na kuitikisa chupa niliona wazo langu
limekubalika na jambo hili lilinifanya nielewe kuwa kazi ya hamasa niliyoifanya
ilikuwa imezaa matunda!
Kutokana na uchunguzi uliofanywa na mwandishi wa makala hii,
Diwani wa Kata ya Kiloleli Manyama ameweza kuwa mwanasiasa wa mwaka 2017
aliyebuni mbinu ya kuweza kupata matokeo ya kile alichokibuni na kushinda kabla
ya kutangazwa kwa matokeo jambo ambalo wengi hata wale ambao wanaweza kuhonga
ili wapigiwe kura imekuwa vigumu kujua nai kampigia kura na nani hakumpigia
kura mpaka baada ya matokeo ndipo wanapokuja kupata matokeo.
Katika Uchaguzi huo uliofanyika Desemba 5, 2017 katika uwanja wa
CCM Kambarage Mjini Shinyanga,Mabala Mlolwa aliibuka kidedea baada ya kuwabwaga
washindani wake ambapo Mlolwa alipata kura 702
John Festo Makune kura 35 na Cornel Ngudungi akiambulia kura 02.
Msimamizi wa uchaguzi na mlezi wa Chama hicho Mkoani Shinyanga
Abdallah Juma Magodi ambaye pia ni Naibu
Katibu Mkuu Chama Cha Mapinduzi (CCM) Zanzibar alimtangaza Mabala Mlolwa kuwa
ndiye mshindi wa nafasi ya Mwenyekiti wa Chama cha Mapinduzi Mkoa wa Shinyanga.
“Naomba kusoma matokeo ya kazi tuliyoifanya,Ndugu Mabala Mlolwa
kura 702 Ndugu John Festo Makune kura 35
na Cornel Ngudungi kura 02.
“Hivyo kwa mamlaka niliyopewa ya kuwa msimamizi wa Uchaguzi huu
namtangaza ndugu Mabala Mlolwa kuwa ndiye Mwenyekiti wa Chama cha Mapinduzi
Mkoa wa Shinyanga.”alisema Abdallah.
Kwa nafasi ya mjumbe wa Halmashauri Kuu ya CCM Taifa
ikichukuliwa na Gaspar Kileo aliyepata
kura 702 dhidi ya wapinzani wake Bernad Shigela aliyepata kura 33 na
Joyce Masunga-02.
Joyce Masunga-02.
Diwani wa Kata ya Kiloleli Mh Manyama akiwa na Diwani wa Viti
Maalumu pamoja na Mbunge wa Jimbo la Kishapu Mh Suleiman Nchambi mwenye fimbo
wakijadili jambo wakiwa na chupa ya chai iliyokuwa ndiyo kivutio cha wajumbe wa
Mkutano Mkuu wa Mkoa wa Shinyanga wakiwa kwenye Uchaguzi wa chama hicho Uwanja
wa Kambarage Mkoani Shinyanga. Picha na
Antony Sollo.
Wajumbe wakiwa wanaendelea na zoezi la upigaji kura katika
ukumbi wa Uwanja wa Kambarage Mkoani Shinyanga.
Mwenyekiti wa CCM Mkoa wa
Shinyanga Mabala Mlolwa akitoa shukrani
kwa wajumbe walimpigia kura baada ya matokeo: Picha na Antony Sollo
Mjumbe wa NEC Ndugu
Gasper Kileo akitoa shukrani baada ya kutangazwa mshindi wa nafasi hiyo: Picha na Antony Sollo
Wajumbe wakiwa wanaendelea na zoezi la upigaji kura katika
ukumbi wa Uwanja wa Kambarage Mkoani Shinyanga. Picha na Antony Sollo.
Mkuu wa Mkoa wa
Shinyanga Zainab Telak akiwa na msimamizi wa Uchaguzi na mlezi wa Chama cha
Mapinduzi Mkoa wa Shinyanga ndugu Abdallah
Juma Magodi ambaye pia ni Naibu Katibu
Mkuu Chama Cha Mapinduzi (CCM) Zanzibar Picha na Antony Sollo.
No comments: