Kutoka IKULU: Waziri Mkuu Mstaafu Mzee Cleopa David Msuya Atangaza Rasmi Kung’atuka Nafasi Zote Za Uongozi Baada ya Kuitumikia Serikali na Chama Cha Mapinduzi(CCM)Kwa Zaidi ya Miaka 33
Rais Dkt.Jakaya Mrisho Kikwete
akiteta jambo na Waziri mkuu Mstaafu mzee Cleopa David Msuya
aliyetangaza rasmi kung’atuka nafasi zote za uongozi baada ya
kuitumikia serikali na Chama Cha Mapinduzi(CCM) kwa zaidi ya miaka
33.Mzee Msuya alitangaza hayo katika hafla maalumu iliyofanyika katika
ofisi kuu ya Chama Cha Mapinduzi wilayani Mwanga
Wazee
wa wilaya ya Mwanga wakimkabidhi Mzee Cleopa David Msuya zawadi
mbalimbali na kumkaribisha kijijini wakati wa hafla ya kumuaga kama
kiongozi iliyofanyika katika ofisi kuu ya CCM Wilayani Mwanga jana
Waziri
Mkuu Mstaafu mzee Cleopa David Msuya akitoa hotuba yake mjini Mwanga
jana wakati wa hafla ya kumuaga baada ya utumishi wa umma wa muda mrefu.
Rais Dkt.Jakaya Mrisho Kikwete
akimpongeza na kuzungumza na Waziri mkuu Mstaafu mzee Cleopa David Msuya
aliyetangaza rasmi kung’atuka nafasi zote za uongozi baada ya
kuitumikia serikali na Chama Cha Mapinduzi(CCM) kwa zaidi ya miaka
33.Mzee Msuya alitangaza hayo katika hafla maalumu iliyofanyika katika
ofisi kuu ya Chama Cha Mapinduzi wilayani Mwanga
Rais Dkt.Jakaya Mrisho Kikwete,
Waziri Mkuu mstaafu Mzee Cleopa David Msuya wakiwa katika picha ya
pamoja na viongozi wengine wa Chama na Serikali wakati wa hafla ya
kumuaga iliyofanyika katika ofisi kuu ya CCM mjini Mwanga,Mkoani
Kilimanjaro jana ambapo Mzee Msuya alitangaza kung’atuka rasmi kutoka
nafasi zake zote za uongozi wa umma.Wengine katika picha walioketi mbele
kutoka kushoto ni Mkuu wa mkoa wa KilimanjaroBwana Leonidas
Gama,Mwenyekiti wa CCM Mkoa wa Kilimanjaro, Katibu Mkuu wa CCM Ndugu
Abdulrahman Kinana, na kulia ni Waziri wa maji mbaue pia ni mbunge wa
Mwanga Profesa Jumanne Maghembe.
No comments: