Ads Top

FUJO ZA 30.8.2014 KATIKA SHOW YA DIAMOND HASARA EURO 300,000 PROMOTER MATATANI

 
 So-called promoter Awin Williams Akpomiemie.
 Hali ya ukumbi baada ya fujo

 Msanii Diamond akiondolewa chupu chupu katika mikono ya wenye hasira hivi karibuni

FUJO ZA 30.8.2014 KATIKA SHOW YA DIAMOND HASARA EURO 300,000
PROMOTER HAKUWA NA BIMA 

PROMOTER BRITTS EVENT MATATANI MJINI STUTTGART,UJERUMANI
Polisi wamesema mpaka kieleweke, M-Nigeria Roho Juu
Stuttgart,Ujerumani,
Anayejiita promota Biritts Event - inayomilikiwa na Awin Williams Akpomiemie raia wa Nigeria amejikuta katika mashaka baada ya ripoti ya polisi kuthibitsha jumla ya hasara ya Euro 300,000(Tsh.600 Million) zilizo sababishwa na fujo ya siku ya jumamosi 30 Augost 2014 baada ya msanii wa NASIB ABDUL AKA DIAMOND PLATINUMZ kuchelewa kufika ukumbini mjini Stuttgart,ujerumani.
Baada ya uchunguzi wa polisi kufuatia fujo hizo imegundulika kuwa muandaaji wa onyesho hilo Mr.Awin Williams Akpomiemie aliudanganya utawala wa ukumbi wa Sindfingen kwa kukodisha ukumbi huo kwa ajili ya african paty na mkutano sio onyesho la muziki kama alivyofanya,na kusababisha fujo zilizotia hasara ya euro 300,000 ( T-shilingi millioni 600=) ambazo inatakiwa alipe,kwa promota huyoAwin Williams Akpomiemie hakuwa na bima ya ku-cover au kulinda onyesho hilo na ukumbi lilipofanyika ambapo ni ukumbi wa mikutano na maonyesho ya bidhaa siyo muziki.

taarifa za uhakika polisi imelipeleka swala hilo kwa ofisi ya sheria (Stadt Anwalt)
ya mji wa Stuttgart ili ichukue mkondo wa sheria ambao unamweka roho juu
bwana Awin Williams Akpomiemie - BRITTS EVENTS, Polisi inaendelea 
kumuhoji kwa kujihusika na biashara zingine haramu.

Wakati huo huo tahasisi mbali mbali na jumuiya za wafrika nchini ujerumani na jirani zimelaani vikali tabia za raia huyo wa nigeria Awin Williams Akpomiemie za kuwadanganya washabiki na kulivunjia adhi sifa za bara la Afrika nchini ujerumani ,tahasisi na jumuiya hizo zimewaonya watu kujiepusha kabisa na m-nigeria huyo Britts Events au Awin Williams Akpomiemie,Pia magazeti mbali mbali ya ujarumani na nchi za kiafrika yameandika BRITTS MAFIA HITS STUTTGART,GERMANY AGAIN !! mojawapo ya gazeti la ghana soma; http://www.modernghana.com/news/567209/1/african-diaspora-is-still-bleeding-diamonds-nightm.html

No comments:

UHURUTZ. Theme images by hanoded. Powered by Blogger.