Ads Top

Taarifa kutoka mjini Mogadishu nchini Somalia, mlipuaji wa kujitoa mhanga amejilipua na kuwaua watu 12 katika msafara wa majeshi ya Muungano wa Afrika

 
Mshambuliaji huyo wa kujitoa mhanga aligongesha gari alilokuwa anaendesha likiwa na mabomu kwenye msafara huo karibu na mji wa Afgoye Kaskazini Mashariki ya mji mkuu Mogadishu.


Wengi waliouawa walikuwa raia waliokuwa wanasafiri kwenye basi la abiria.


Zaidi ya watu 20 wameripotiwa kujeruhiwa. Mji huo umekuwa kitovu cha mashambulizi yanayofanywa na wanamgambo wa Al Shabaab.


Shambulizi hili limetokea siku chache baada ya Marekani kuthibitisha kumuua kiongozi wa Al Shabaab Ahmed Gofane.


Kadhalika kundi hilo lilikuwa limesema kuwa litalipiza kisasi mauaji ya kiongozi wake ila halikusema eneo ambalo watashambulia.

No comments:

UHURUTZ. Theme images by hanoded. Powered by Blogger.