Ads Top

Wazazi wa Somalia wanachukua jukumu kubwa zaidi katika kushawishi watoto wao kutofuata itikadi ya msimamo mkali

Mwili wa mpiganaji wa al-Shabaab Adan Sheikh Abdi unachukuliwa tarehe 1 Agosti 2013, baada ya kuuawa na kundi lililofyatua risasi katika uwanja wa Mogadishu kwa ajili ya mauaji ya Septembea 2012 ya mwandishi wa habari wa Somalia Hassan Yusuf Absuge. Abdi alihukumiwa kifo mwezi Machi 2013 na rufaa yake iliyofuatia ilikataliwa. [Mohamed Abdiwahab/AFP]
Mwili wa mpiganaji wa al-Shabaab Adan Sheikh Abdi unachukuliwa tarehe baada ya kuuawa na kundi lililofyatua risasi katika uwanja wa Mogadishu kwa ajili ya mauaji ya Septembea 2012 ya mwandishi wa habari wa Somalia Hassan Yusuf Absuge. Abdi alihukumiwa kifo mwezi Machi 2013 na rufaa yake iliyofuatia ilikataliwa.


Mahakama ya kijeshi ya Somalia imetekeleza mauji ya watu wapatao tisa ya wanachama wa al-Shabaab waliotiwa hatiani katika kipindi cha miezi miwili iliyopita, na kushughulikia hukumu ya kifo na kifungo cha maisha kwa wengine wengi.


 Mahakama pia imeonya wazazi dhidi ya kujifanya vipofu kwa watoto wao wanaojihusisha na kikundi cha kigaidi, na kuwataka kuchukua jukumu kubwa zaidi katika kupambana na ueneaji wa itikadi ya al-Shabaab. 

"Hofu kubwa tulio nayo ni kwa watoto wetu kukubali itikadi ya msimamo mkali wakati huu ambao wakala wa mahakama wa taifa inaongeza hukumu wanayoitoa kwa al-Shabaab," alisema Asha Mohamed, mama mwenye umri wa miaka 51 mwenye watoto wanane na mkaazi wa wilaya ya Hamar Jajab ya Mogadishu.

"Kila siku asubuhi kabla ya kuwapeleka watoto shule, huwa nawaambia wawe makini na yeyote ambaye wanamhisi anajihusisha na itikadi isiyo sahihi ya al-Shabaab," aliiambia Sabahi.

Mohamed alisema aliweka jitihada kubwa katika kuwaasa watoto wake kuhusu matokeo mabaya ya msimamo mkali, na pia anatumia muda kuelewa kuhusu watoto wengine wanaoshinda na watoto wake.

Farah Muse, mwenye miaka 48 baba wa watoto sita katika wilaya ya Waberi huko Mogadishu, alisema pia amekuwa akifanya jitihada za ziada kuzungumza na watoto wake kuhusu msimamo mkali na kuelewa kuhusu wanafanya nini na marafiki wanaokuwa nao wakati hawako nyumbani.

Itakuwa ni hali ya kutisha kwa mzazi kujua kwamba mmoja wa watoto wake amejiunga na al-Shabaab bila ya wao kujua au amekamatwa kwa uhalifu unaohusiana na ugaidi, alisema.

"Hilo ndio limenisababisha nitumie muda mwingi katika kuwaelimisha watoto wangu dhidi ya imani za magaidi na ninatumia njia ya dini ili watoto waweze kuelewa kwamba itikadi ya ugaidi haina msingi katika dini ya Kiislamu," aliiambia Sabahi.

Muse alitoa wito kwa wanazuoni wa Kiislamu kujihusisha katika kutoa utambuzi kuhusu itikadi ya ugaidi yenye makosa na ya kujiangamiza wenyewe . "Jamii inapaswa kushirikiana kupambana na itikadi hiyo na nafikiri njia pekee ya kupambana nayo ni kupitia kampeni za uelimishaji zinazoendelea," alisema.

 
Amina Hussein, mwenye umri wa miaka 42 na mama wa watoto saba huko wilaya ya Hamarweyne, alisema anapongeza jitihada za kupambana na itikadi ya msimamo mkali, lakini aliiomba mahakama ya kijeshi kutotangaza mauaji kwenye televisheni. 

"Ningependa kuiomba serikali ya Somalia kuacha kuonyesha picha za watu ambao wanatarajia kuuawa wakati wamefungwa ili kupigwa risasi kufa kwa kuwa kufanya hivyo kunaweza kuwapa hofu wazazi [wao]," aliiambia Sabahi.

"Hakuna mtu angependa kuona mtoto wake akijiunga na al-Shabaab," alisema, akiongeza kwamba kutangaza mauaji katika televiseni hakutakiwi kuwashawishi wazazi kushirikiana na mamlaka na kuripoti watoto wao wanaoonyesha dalili za msimamo mkali.

Hata hivyo, Hussein alitoa wito kwa wazazi kutimiza wajibu wao na kutahadharisha mashirika ya usalama mara wanapomshuku mtoto wao kuwa ni mwenye msimamo mkali wajue kwamba maisha yake na maisha ya wengine yameokolewa.
 
"Wazazi wengi wanajisikia kwamba kama watatoa taarifa kuhusu watoto wao wanapowashuku kuwa wanajifunza kuwa wenye itikadi kali watatendewa vibaya," alisema. "Hata hivyo, ningewashauri kuwahadharisha mashirika ya usalama dhidi ya shughuli za watoto kabla ya kufanya uhalifu ambao utasababisha kushitakiwa au kuhukumiwa kifungo cha jela kwa muda mrefu."

Kwa upande wake, mstaafu wa Jeshi la Somalia Kanali Dahir Timaadde alisema kuwapiga al-Shabaab kutategemea ama jamii kutoa au kutotoa ushirikiano kamili katika jitihada za serikali kushughulikia kikamilifu magaidi.

Alisema Wasomali wanapaswa kuunga mkono hukumu ya kifo kwa wale wanaofanya vitendo vya kigaidi ili kuwazuia wengine na kuokoa maisha ya umma kwa ujumla.

"Ninawashauri wazazi ambao wana wasiwasi kuhusu watoto wao kukubali itikadi ya msimamo mkali kuwapeleka wakala ya mashirika ya usalama ili waweze kupelekwa katika vituo vya kuwawezesha kuishi maisha ya kawaida kwa ajili ya wasaliti wa al-Shabaab," aliiambia Sabahi.

Wakati huohuo, Timaadde alitoa wito kwa serikali ya Somalia kuongeza idadi ya vituo vya urekebishaji ili wazazi wajisikie kuwa na uhakika kwamba watoto wao watapata huduma wanayoitaka watakapowaripoti.

No comments:

UHURUTZ. Theme images by hanoded. Powered by Blogger.