Fundi Haule akiwa amelala bila kujitambua baada ya kupigwa na kuburuzwa kama mzigo.…Akiwa anachuruzika damu na kugumia kwa maumivu.Wananchi waliofika eneo la tukio.… Haule (katikati) akipelekwa hospitali baada ya ndugu zake kujitokez KIJANA mmoja aliyetambulika kwa jina moja la Haule ambaye ni fundi seremala amepata kipigo cha nusu ya kufa kutoka kwa mteja wake aliyedaiwa ni mwanajeshi na ambaye aliongozana na wanajeshi wenzake wawili kumshambulia. Tukio hilo la aina yake lililosababisha wananchi kibao kujitokeza sehemu hiyo, limetokea maeneo ya Magomeni-Morocco jijini Dar es Salaam ikiwa ni siku ya tatu kupokea dozi hiyo iliyomuacha akiwa mahututi huku damu zikimtoka baada ya watu watatu waliojitambulisha kuwa ni wanajeshi kumshushia kipigo kutokana na mmoja wao kumdai kitanda ambacho alishamlipa laki tatu ili amtengenezee. Baada ya kumshushia kipigo fundi huyo, wananchi walijitokeza ambapo walifanikiwa kuwakamata wanajeshi wawili na kuwapeleka katika kituo cha polisi Magomeni huku mmoja akifanikiwa kuwatoroka, jambo ambalo lilisababisha machafuko ya muda mrefu ambapo polisi walichelewa kufika eneo la tukio.
No comments: