Ads Top

MAGUNIA YA BANGI YALIYOKAMATWA NA POLISI‏ MPAKANI MWA KENYA NA TANZANIA




Askari polisi wakiangalia magunia 50 ya madawa ya kulevya aina ya bangi yaliyokamatwa Mei 23 mwaka huu, majira ya saa 9 alasiri katika kijiji cha Sinya milima saba, mpakani mwa Kenya na Tanzania. Polisi wakishirikiana na askari wa wanayamapori waliwakamata watu wanne waliokuwa na magunia ya bangi kwenye gari aina ya Canter lenye namba za usajili T 922 AFJ wakiyasafirisha kutoka wilayani Arumeru kwenda nchi jirani ya Kenya kupitia njia za panya.
Waliokamatwa ni:
1. Babu Laizer (34) mkulima.
2. Lomnyaki Lokibengi (30) mkulima.
3. Jonh Joshua (29) ambaye alikuwa Utingo wa gari hilo.
4. Edward Mollel (27) dereva wa gari.
Watuhumiwa wote wanne ni wakazi wa eneo la Oldonyoi Sambu wilayani Arumeru mkoa wa Arusha.

No comments:

UHURUTZ. Theme images by hanoded. Powered by Blogger.