AMOS MAKALLA AMETOA MILIONI KUMI KWA MAMA WA MAREHEMU KANUMBA
Makalla (kulia) akikabidhi fedha hizo
Mama yake Kanumba akizionyesha fedha hizo
Mama Kanumba, Flora Mtegoa, akiwa na Makalla (katikati) na kulia ni ofisa aliyefuatana na Makalla.
NAIBU Waziri wa Habari, Utamaduni, Vijana na Michezo, Amos Makalla, leo ameiwakilisha serikali kutoa rambirambi ya shilingi milioni 10, kwa familia ya aliyekuwa mwigizaji, marehemu Steven Kanumba nyumbani kwa marehemu Sinza Vatican, jijini Dar.
Mbali na kutoa rambirambi, Makalla alisisitiza kuwa kifo cha Kanumba kimeleta chachu na kuahidi kuwa serikali itajikita kikamilifu kusimamia kuboresha pato la wasanii.
No comments: