Ads Top

MZEE SMALL TAABANI KITANDANI

MDOGO WAKE ASIMULIA
“Kwa kuwa ilikuwa usiku nilishindwa kwenda lakini kesho yake nikawahi. Nilimkuta kama mtu aliyechanganyikiwa, midomo yake ikapinda, akawa hawezi kuongea.
“Mkono wake mmoja ulikuwa ukishindwa kufanya kazi sawasawa kama mkono mwingine, hali hiyo ilitupa wasiwasi.
ALIVYOSEMA DAKTARI
Mdogo wake huyo akaendelea kusema: “Ikabidi tumkimbize Hospitali ya Amana ambapo daktari mmoja baada ya kusikia maelezo yetu na jinsi mgonjwa alivyo, alisema ana dalili zote za kiharusi ‘stroke’ hivyo akalazwa kwa ajili ya uchunguzi zaidi,” alisema Karim.
MWANZA ALIFUATA NINI?
Safari ya Mzee Small jijini Mwanza akiwa ameambatana na mkongwe mwenzake, Bi. Chau ilikuwa kwa ajili ya kufanya kampeni maalumu ya watu wenye ulemavu wa ngozi iliyofanyika katika Chuo cha Bungando jijini humo.
NENO LA MHARIRI

Ni kipindi kingine ambacho Watanzania kwa umoja wetu tunatakiwa kumwomba Mungu ili amrejeshee afya Mzee Small ambaye ana mchango mkubwa katika jamii.

No comments:

UHURUTZ. Theme images by hanoded. Powered by Blogger.