China: Ni mwekezaji au mporaji?
Waekezaji wa China Afrika
Uwekezaji wa China barani Afrika, umeendelea kukuwa kwa kasi katika miaka ya hivi karibuni. Lakini nini athari za hatua ya China barani humo?Uchumi wa China ni mkubwa sana. Ndoto yake kubwa ikiwa kuekeza zaidi barani Afrika. Kama Brazil , Urusi na India, China itaendelea kukita mizizi barani afrika kwa miaka mingine mingi ijayo.
Kuhoji ikiwa China ni nzuri au mbaya kwa Afrika, sio swali la pekee muhimu. Swali hili linasukuma mawazo yetu kutoka kwa mambo mangine muhimu kama vile, nini hasa ambacho hizi nchi za Afrika zinataka kutoka kwa ushirikiano huu mpya na wanafanya nini kuweza kufaidika zaidi?
China sasa ndiye mshirika mkubwa wa kibiashara barani Afrika, imeshinda Marekani na Ulaya. Ushirikiano wa kibiashara kati ya kanda hizi mbili, ulianza tangu mwaka 2000, kutoka kwa dola bilioni 10 na kufika dola bilioni 100 katika miaka kumi iliyopita.
Jengo jipya la makao makuu ya muungano wa Afrika mjini Addis Ababa Ethiopia, ilikuwa zawadi ya thamani ya dola milioni 200 kutoka kwa Bijing kwa mataifa ya Afrika.
Hii bila shaka ilikuwa dalili ya nia ya China na uwezo wake kushirikiana na nchi za Afrika na hata bara zima kwa ujumla kwa kuzipa changamoto kubwa pamoja na uwezo mkubwa.
Ushirikiano wa kibiashara wa China na Afrika ikitafsiriwa kwa takwimu
Kukithiri kwa ushirikiano wa kibiashara kati ya China na Afrika, imewafanya wakosoaji wengi hasa kutoka mataifa ya magharibi, kuhoji nia na malengo ya China.
Je uwekezaji unakaribishwa?
Wakati wengi wakihoji kwamba China ndio mshirika mkubwa zaidi wa karne ya 21 wa maendeleo na mchochezi mkubwa wa ukuwaji, wakosoaji wanahofia kuwa China ni mkoloni mpya mkubwa.
Na kikubwa inachotaka tu ni kupora mali asili ya Afrika na kuendeleza ufisadi na umaskini.
Biashara za China barani Afrika na washirika wake wakubwa
1. Angola: dola bilioni 24.8
2. South Africa: dola bilioni 22.2
3. Sudan: dola bilioni 8.6
4. Nigeria: dola bilioni 7.8
5. Egypt: dola bilioni 7.0
Hata hivyo kuna watetezi wa China ambao wanasema kuwa nchi hiyo imefaidi sana bara la Afrika , kupitia uwekezaji wake mkubwa na kurejesha imani katika masoko madogo ya Afrika pamoja na kuleta manufaa kwa chumi za Afrika. .
Licha ya ukosoaji mkubwa kutoka pembe zote hasa vyombo vya habari vya nchi za magharibi, hali halisi ni kwamba vyovyote ungependa kuitizama China, serikali na wananchi wa nchi za Afrika, wanakaribsha uwekezaji wa China barani Afrika.
China Afrika
Hii ni kauli iliyotolewa na meneja mkuu kutoka tume ya kiuchumi ya umoja wa mataifa.
Hata hivyo ushirikiano huu una changamoto zake na mambo sio shwari kama ambavyo vyombo vya habari vya mataifa ya Asia hutaka kuonyesha.
Ukweli ni kwamba uhusiano wa China na nchi za kiafrika sio shwari vile. Lakini ni kweli kuna changamoto tele na sio wazi hali itakavyokuwa katika siku za usoni.
Cha kwanza ni kwamba China hufanya shughuli zake kivyake sio kama kanda.
Ukweli ni kwamba uhusiano wa China na nchi za kiafrika sio shwari vile. Lakini ni kweli kuna changamoto tele na sio wazi hali itakavyokuwa katika siku za usoni.
Cha kwanza ni kwamba China hufanya shughuli zake kivyake sio kama kanda bali nchi hiyo inaendeshwa na waekezaji wa binasfi, mashirika ya kiserikali na wafanyabiasha wachina walio barani Afarika na ambao hushindana wenyewe ka wenyewe pasipo kujali kauli mbiu ya taifa hilo la kikomunisti. .
Raia wa Zambia waelezea a uwekezaji wa China nchini mwao unawaathiri.......kwenye mjadala wetu saa kumi na mbili na nusu jioni
Afrika mashariki.
No comments: