KIGOGO ANATAKA KUWAUWA DK SLAA,MNYIKA,MBOWE ASEMA MPANGO HUO UNARATIBIWA NA KIGOGO WA USALAMA WA TAIFA, MKUCHIKA ASEMA NI TUHUMA NZITO
Mwenyekiti wa Chadema (kulia)Freeman Mbowe akiwa na kada wa CCM Sabodo
CHAMA cha Demokrasia na Maendeleo (Chadema),kimetoa tuhuma nzito kikidai kigogo mmoja (jina tunalo) wa Idara ya Usalama wa Taifa anaratibu mpango wa kuwaua viongozi wake waandamizi akiwamo Katibu Mkuu, Dk Willbrod Slaa na Mbunge wa Ubungo, John Mnyika.
Kwa sababu hiyo, chama
hicho kimeitisha kikao cha Kamati Kuu (CC) leo kujadili mambo mbalimbali
na Mwenyekiti wake, Freeman Mbowe amesema ajenda kuu itakuwa
kuzungumzia usalama wa viongozi wao kutokana na vitisho hivyo.
Kuhusu
tuhuma hizo, Waziri wa Nchi, Ofisi ya Rais (Utawala Bora), George
Mkuchika amesema tuhuma hizo ni nzito na atazijibu kwa maandishi.
Katika
mkutano wake na waandishi wa habari uliofanyika Dar es Salaam jana,
Mbowe alitaja majina ya baadhi ya maafisa idara hiyo (majina
tunayahifadhi) na kudai kuwa mmoja kati yao ndiye anayeratibu shughuli
hiyo na tayari yupo mjini Dodoma kwa ajili ya kuongoza kundi linalotaka
kumdhuru Mnyika.
Mbowe ambaye pia ni Kiongozi wa Kambi ya
Upinzani Bungeni, alisema mbali na viongozi hao wawili, mwingine
aliyedai kuwa anafuatiliwa ni Mjumbe wa Kamati Kuu, Godbless Lema akidai
kwamba, taarifa zinaonyesha kuwa wanafuatiliwa kwa saa 24.
Mbowe
alidai kwamba idara hiyo ambayo haifanyi shughuli za siasa, inatumia
ofisi yake vibaya kwa kufuatilia viongozi hao wakidhani chama hicho kina
mambo ya siri kinayotaka kuyafanya katika nchi hii.
“Sisi Chadema
hatuna mambo ya siri tunayotaka kufanya katika nchi hii. Matatizo ya
Watanzania yapo wazi na yanajulikana na kila mmoja, Serikali ya CCM
itekeleze sera na ahadi zao kwa wananchi na si vitisho,” alisema Mbowe
na kuongeza:
“Tunaomba wananchi waelewe kuwa viongozi wao wako
hatarini, lakini Chadema hatutarudi nyuma katika kutetea haki za
wanyonge hata kwa kufa na hatuwezi kupeleka malalamiko yetu polisi
sababu nao ni sehemu ya tatizo.”
Alisema chama chake kimekuwa
kikihusishwa na mambo mengi ukiwamo mgomo wa madaktari unaoendelea na
kusema Chadema hakiko nyuma ya mgomo huo na hakijawahi kukutana na
kufanya kikao na madaktari.
“Wametuhusisha na mambo mengi na sasa
wanasema tuko nyuma ya mgomo wa madaktari, taarifa hizo siyo za kweli na
wala hatujawahi kukaa nao kikao chochote kujadili masuala yao,
madaktari wana madai ya haki zao. Hapa tunaingia kwenye utaratibu wa
kutesana ili kupata taarifa, mmesikia Dk Ulimboka aliteswa ili aseme
Chadema iko nyuma ya mgomo,” alidai Mbowe.
Hata hivyo, Mbowe
alisema suala la kutokuwa nyuma ya mgomo huo haliwanyimi fursa ya
kutetea makundi ya watu wanaodai haki zao wakimwamo madaktari na kusema
anaunga mkono tamko la viongozi wa dini.
“Viongozi wa dini wametoa
tamko lao jana (juzi), wakitaka Serikali kuwarudisha madaktari na
kumalizia suala hilo kwa njia ya mazungumzo,” alisema.
Alisema Chadema kinaunga mkono tamko hilo akisema si busara kuwa fukuza kwa sababu Serikali imetumia gharama kuwaandaa.
Dk Slaa anena
Kwa upande wake, Dk Slaa alisema Chadema kimeamua kutotoa madai yake polisi akidai kuwa imepokea madai mengi kutoka kwa viongozi na wanachama ya kutendewa visivyo lakini hakuna hata moja lililowahi kufanyiwa kazi.
Kuhusu kitisho la kuuawa alidai kwamba alianza kutishiwa siku nyingi na kusisitiza kuwa hilo haliwezi kuwanyamazisha.
Kwa upande wake, Dk Slaa alisema Chadema kimeamua kutotoa madai yake polisi akidai kuwa imepokea madai mengi kutoka kwa viongozi na wanachama ya kutendewa visivyo lakini hakuna hata moja lililowahi kufanyiwa kazi.
Kuhusu kitisho la kuuawa alidai kwamba alianza kutishiwa siku nyingi na kusisitiza kuwa hilo haliwezi kuwanyamazisha.
“Taarifa
za sasa wanaanza na Mnyika na kufuatia mimi, ninachosema wafanye
watakavyo hatutaacha kufanya kazi yetu, hata nilipoibua tuhuma za EPA
niliwaambia watuhumiwa wengine wa sakata hilo ni Usalama wa Taifa,”
alisema Dk Slaa.
Dk Slaa alitaja baadhi ya mambo ambayo alidai
kuwa hayakushughulikiwa yalipowasilishwa polisi kuwa ni vinasa sauti
alivyowekewa kwenye chumba alichokuwa amelala wakati wa vikao vya Bunge
Mjini Dodoma.
Alisema vifaa hivyo vilichukuliwa na polisi kwa
ajili ya kufanyiwa uchunguzi lakini hadi leo hakuna taarifa iliyotolewa
hata kwake licha ya kuwa mhusika mkuu.
Mnyika: Namwachia Mungu
Akizungumzia madai hayo, Mnyika alisema anamuachia Mungu kwa kuwa ndiye aliyetoa uhai hata kwa hao wanaofikiria kutekeleza kitendo hicho.
Akizungumzia madai hayo, Mnyika alisema anamuachia Mungu kwa kuwa ndiye aliyetoa uhai hata kwa hao wanaofikiria kutekeleza kitendo hicho.
Mnyika
alidai kuwa baada ya kupata taarifa hizo ambazo alisema zimeandaliwa kwa
ama kunyeshwa sumu au kuvamiwa na majambazi, alikutana na familia yake
na uongozi wa chama chake ambao kwa pamoja wamemtaka aendelee na kazi ya
kutetea rasilimali za taifa.
“Nilipopata taarifa hizi nimekutana
na viongozi wangu wa chama na jana usiku (juzi), nilikutana na familia
yangu, kwa pamoja wameniambia niendelee na kazi hii ninayoifanya kwani
nimetumwa na wananchi na sauti ya wengi ni sauti ya Mungu, ”alisema
Mnyika.
Kwa upande wake, Lema alisema taarifa za kufuatiliwa na
watu hao wanaodaiwa kuwa ni wa Usalama wa Taifa alizipata kwa mmoja wa
vyanzo vyake kutoka serikalini.
“Nilipigiwa simu na mtu mmoja
kutoka serikalini aliyeniambia kuna gari nyuma linanifuatilia,
nilipogeuka niliona na kusimama kisha nikashuka na kubadili gari na
lenyewe likaendelea kunifuatilia katika gari nililokuwa nimepanda,”
alidai Lema.
Lema alidai kwamba hata juzi asubuhi alikutana nalo katika nyumba aliyofikia na alipolikaribia watu hao walishusha vioo na kumsalimu wakimwita ni Mbunge wa Arusha aliyeko kwenye likizo.
Lema alidai kwamba hata juzi asubuhi alikutana nalo katika nyumba aliyofikia na alipolikaribia watu hao walishusha vioo na kumsalimu wakimwita ni Mbunge wa Arusha aliyeko kwenye likizo.
No comments: