JINSI WATUHUMIWA WA VURUGU MBAGALA WALIVYOFIKISHWA MAHAKAMANI JIJINI DAR ES SALAAM
Magari yaliyotumika kuwafikisha washitakiwa waliofanya vurugu, uaribifu na wizi wa mali za makanisa Mbagala, wakiwasili katika Mahakama ya Hakimu Mkazi Kisutu kujibu mashitaka yanayowakabili.
Washitakiwa wa kike katika kesi hiyo wakielekezwa kuingia kwenye ukumbi wa mahakama.
Baadhi ya washitakiwa hao wakipanda basi la polisi kurejea mahabusu baada ya kumalizwa kutajwa kwa kesi yao.
Hapa wakiwa wamewekwa chini ya ulinzi mkali wa polisi kabla ya kuingia katika moja ya ukumbi mahakamani hapo
Washitakiwa hao wakiwa katika picha ya pamoja baada ya kuingizwa kwenye ukunmbi wa mahakama.
Mmoja wa askari akiwa katika ulinzi mkali wa kulinda gari
lililowapeleka washitakiwa hao mahakamani na kuwarejesha mahabusu
---
DAR ES SALAAM, Tanzania
WATU 37 wakiwamo wanawake wawili
wanaotuhumiwa kuchoma makanisa, kufanya uharibu wa mali na kuiba kwa kutumia
nguvu huko Mbagala Zakhem jijini Dar es Salaam, Ijumaa iliyopita, leo wamefikishwa katika
Mahakama ya Hakimu Mkazi Kisutu chini ya ulinzi mkali.
Washitakiwa hao waliofikishwa mahakamani
hapo
wakiwa kwenye magari matatu ya polisi aina ya Defender majira ya saa
6:26
mchana chini ya ulinzi mkali wa askari waliokuwa wamevalia mabomu
viunoni, kutokana na kufanya matukio hayo kama sehemu ya malipizi yao
kutokana na madai ya kunajisiwa kwa mkojo kwa Msahafu kulikofanywa na
kijana wa Kikristo.
Baada ya kushushwa, watuhumiwa hao
waliamriwa kuchutama kabla ya kuanza kuingizwa kwenye chumba namba moja cha
mahakamani hapo, huku kukiwa na tahadhari kubwa ya kiusalama ndani na nje ya mahakama
hiyo.
Kwa upande wa mashtaka, watuhumiwa hao wamefunguliwa
kesi nne tofauti za jinai kwa mpigo, kesi ya kwanza ni jinai Namba. 240/2012,
namba 241/2012, namba 242/2012 na 243/2012.
Watuhumiwa hao walisomewa mashtaka hayo
mbele ya Mahakimu Wakazi wawili Sundi Fimbo anayesikiliza kesi tatu huku moja
ikisikilizwa na Hakimu Mkazi Bingi Mashabara.
Upande wa Jamhuri kwenye keshi hiyo uliwakilishwa
na Wakili Mwandamizi Tumaini Kweka, Lasdlaus Komanya na Joseph Maugo.
Wakili Kweka alidai katika kesi ya jinai
namba 243/2012 inayowakabili washitakiwa 17 ambao ni Maenga Rwenda, Hamad Euli, Shego Sheso, Ramadhani Mgule,
Mashaka Iman, Kassim Juma Kigoni, Ibrahim Himu, Hamza Fundi Hamza,
Mikidadi Sadick, Juma Mbegu na Rahimu
Boga.
Wengine ni Issa Abdallah, Hamis Kmwaga, Ramadhani Mbulu, Hamed Mohamed, Mohamed
Yusuf na Msha Alifa, wanakabiliwa na kosa la kula njama kutenda kosa la unyang’anyi wa kutumia silaha kinyume na
kifungu cha 287A cha sheria ya Kanuni ya Adhabu ya mwaka 2012.
Wakili Kweka alidai kuwa Oktoba 12, mwaka huu huko Mbagala wajatwa waliiba vitu
mbalimbali ikiwamo 'Laptop', 'Printer Projector', spika, saa za ukutani na viti vya
plastiki vyote vikiwa na thamani ya sh milioni 20 mali ya Kanisa la Kiinjili
la Kilutheli Usharika wa Mbagala.
Imeelezwa mahakamani hapo kuwa, kabla ya
kuiiba watuhumiwa wamtishia mlinzi Michael Samwel kwa mashoka na nondo kwa lengo
la kujipatia vitu hivyo.
Kweka alidai shitaka jingini ni la kuchoma
kanisa kinyume na kifungu cha 319(a) cha sheria ya Kanuni ya Adhabu ambapo
washitakiwa hao kwania ovu walichoma kanisa hilo mali na kuongeza kuwa shitaka
jingine ni la kuharibu mali kama madirisha, meza, mfumo wa umeme, milango, aircondition
vyote mali ya kanisa hilo ambavyo vyote vikiwa na thamani ya sh 500,000,000.
No comments: