UKIUKWAJI WA HAKI ZA BINADAMU NA WANYAMA MKOANI KAGERA
Hapa ndipo yalipokuwa makazi ya Mzee Numbu Yihorogo na sasa anaishi kwa wasamalia wema
Hili ni zizi la Mzee Numbu Yihorogo likiwa halina kitu kwa sasa kufuatia ukiukwaji wa Haki za Binadamu
Mzee Numbu Yihorogo akiwa amebaki peke yake baada ya familia yake kutoweka na sasa hawajulikani walipo
Na Antony Sollo
Kashalunga
Hali iliyopo katika maeneo
mbalimbali Mkoani Kagera inatisha na inatia huzuni kuona Watu sasa tunaelekea
kuanza kubaguana kwa Makabila kinyume na Misingi iliyowekwa na waasisi wa
Taifa letu akiwemo haiyati Baba wa Taifa
Mwalimu Julius Kambarage Nyerere.
Mimi nimepewa taarifa za
matukio haya ya unyama wa kutisha na hatimaye kwenda kuwaona viongozi wa Jeshi
la Polisi Makao Makuu na kufanya mazungumzo yaliyopelekea mimi kuanza safari ya kwenda Mkoani Kagera hususani Wilaya ya Muleba na Biharamuro ili kujionea hali
ilivyo na ili niweze kutoa taarifa za kuaminika katika kituo chetu cha Sheria
na Haki za Binadamu kuhusu maswahibu yanayowakumba wananchi hasa wa Kabila la
wasukuma na baadhi ya makabila machache wanaoishi jirani na Hifadhi mbalimbali
Mkoani humo.
Ndugu zangu,niliyoyaona na
ambayo sasa si ya kusimuliwa,ni kweli nchi yetu inaelekea pabaya kwani
tunaelekea kuanza kubaguana kwa Kabila zetu jambo ambalo ni hatari kuliko
wakati wowote ule katika historia ya Uhuru wan chi yetu.
Huku kuna migogoro mikubwa
inayopelekea shughuli za kijamii zikwame na pia wapo watu sasa wanaishi kama
wakimbizi katika nchi hii ambayo katika medani za kimataifa inasifika kwa
kuwa nchi ya Amani na utulivu jambo ambalo si kweli, kuna familia zinazopata
kufikia idadi ya kaya 1200 wakiwa wamechomewa nyumba zao,na si hivyo tu,kuna
ngombe wanaokadiriwa kufikia 1600 waliopigwa risasi na maafisa wa wanyama
pori Mkoani Kagera jambo ambalo ni ukiukwaji wa Haki za Binadamu pamoja na
wanyama.
Kilichonisikitisha
kuliko yote ni Kupotea kwa wanafamilia ya Mzee Numbu yihorogo ambapo hadi sasa
amebaki maskini wa kutupwa na anaomba msaada wa Wanasheria kutoka kituo cha
Sheria na Haki za Binadamu ili asaidiwe kutoa sauti yake ili serikali iweze
kuwajibishwa kufuatia watumishi wake kufanya unyama kwa raia na mali zao.
Ndugu zangu kuna matatizo
makubwa huku kuna watu wamefuguliwa kesi za kubambikizwa baada ya kukaidi kutoa
rushwa, wapo kina mama na watoto nimeshuhudia wakilala nje na kunyeshewa mvua
na hawana chakula huku waume zao wakijaribu kutoroka kwenda kuangalia mahala pa
kuishi ili kama watafanikiwa waweze kuwarudia ,wapo kina baba niliokutana nao
jana wakitembea kwa miguu wakiondoka maeneo ya makazi walipokuwa wakiishi na
kuelekea huku na kule mithili ya wakimbizi katika nchi yao,na leo wamenipigia
simu kuwa tayari wamefika Chato tena wakitembea kwa miguu, naomba jamani
Uongozi wa Juu wa kituo cha sheria na Haki za Binadamu utafute namna ya kufika
huku na kuweza kutoa msaada wa kisheria kwa kuwapeleka mahakamani watendaji wa
serikali walioshiriki zoezi hili la ukatili kwa raia wan chi hii.
Haya ninayoyasema ninao
ushahidi nimechukua mkanda wa Video sehemu mbalimbali za Mkoa huu ambapo nimuombe
Mkurugenzi wa Kituo cha Sheria na Haki za Binadamu Mama Kijjo atoe tamko kali
maana Bila hivyo huku hakufai wanyarwanda wamewanunua viongozi,wananchi
hawasikilizwi kwa lolote na ninavyoona tutashuhudia maiti nyingi za raia hasa
kina mama na watoto maana wanaachwa na waume zao na wengine hawana hata chakula
na si kwamba wanaachwa kwa makusudi wakina baba wengine wamewekwa mahabusu na
wana kesi mahakamani hata dhamana hairuhusiwi .
Kwa kweli huu ni ukatili wa
kutisha Shime wanaharakati wenzangu nawaomba tuungane tuweze kuwaokoa
watu hawa maana hali ni Mbaya kibaya zaidi hata mawasiliano ni shida sana hasa
katika maeneo ya tukio
No comments: