HAKIMU WA MAHAKAMA YA MWANZO TINDE MKOANI SHINYANGA AFANYA UKATILI KWA MAMA NA MTOTO WA MWAKA MMOJA NA MIEZI MITATU.
Hakimu wa Mahakama ya Mwanzo
Tinde Mkoani Shinyanga leo tarehe 30/11/2012 amefanya ukatili kwa
familia ya John Makomba kwa kuamua kutumia vibaya Mamlaka aliyopewa na
kuutumikia Mhimili huo muhimu baada ya Wakazi wa kijiji cha Tinde
kugombana na hatimaye kushitakiana katika mahakama hiyo.
Akizungumzia suala hili mtoa
taarifa hizi ambaye hakutaka kutajwa jina lake kupitia taarifa
hii amesema, wanafamilia hao walipatwa na maswahibu hayo baada ya
kutokea ugomvi kati ya mke wa John Makomba na Binti mmoja aliyetajwa kwa
jina moja la Anna ambapo imeelezwa kuwa walikuwa wamechelewa kufika
Mahakamani hapo jambo ambalo lilipelekea Hakimu Denis wa Mahakama ya
Mwanzo Tinde kuwaweka ndani wanandoa hao lakini ikwa ni ukiukwaji wa
Sheria.
Majirani wa wanandoa hao
wamesema kuwa wameshtushwa na kilio kilichokuwa kimeiandama nyumba ya
Bwana na John Makomba na walipotaka kujua kulikoni waliambiwa kuwa mama
wa mtoto huyo pamoja na mmewe walikuwa wamewekwa Mahabusu katika Mahakama ya
Mwanzo Tinde kwa kosa la kuchelewa kufika mahakamani.
Habari
zilizotolewa na ndugu wa karibu wa John Makomba zinadai kuwa kuchelewa
kufika mahakamani kwa wanandoa hao kulitokana na kushindwa kupata fedha
mapema shilingi 100,000/= ambazo waliombwa kama Rushwa ili kupata
dhamana na Mh Denis ambapo baada ya kuzipata walianza
safari ambapo walipofika tu waliamuriwa kuwekwa Mahabusu kwa kosa la
kudharau Mahakama.
Nilipomtafuta Mh Denis
kuzungumzia suala hili hakupatikana namba yake ilikuwa
imezimwa na alikuwa Mjini Shinyanga kwa shughuli za Kikazi.
Kinachozidi kuikoroga akili
yangu mpaka sasa ni juu ya kuwekwa Mahabusu familia yote wakati
waliokuwa na ugomvi ni wanawake kwa wanawake lakini pia bila kujali Haki
ya Mtoto mdogo mwenye umri wa miaka mitatu najiuliza Mh Denis sijui
ameupata wapi ujasiri wa kuitumia vibaya sheria namba 96 kuwakandamiza
wanafamilia hawa.
Nilipowasiliana na Mkuu wa Kituo
cha Polisi Tinde alikiri kupokea nyaraka zilizokuwa zimeidhinishwa na
Hakimu huyo ili kuwapeleka Gerezani wanafamilia hao pamoja na watu
wengine na baada ya mazungumzo alisema kuwa suala hili liko kwenye
Mhimili ambao nao una mamlaka kamili yanayotambuliwa na asingeweza
kuingilia maamuzi ya Mhimili huo kwani kila Mhimili unajitegemea kwa
mujibu wa sheria.
Ninachohitaji kutoka kwenu ndugu
zangu ni kujua kuwa Iwapo Hakimu wa Aina hii ataamua kuitumia vibaya
Ofisi yake maamuzi yake hayakubaliki kupingwa? binafsi naona Haki za
Binadamu kwa wanandoa hawa zimekiukwa na si hivyo tu,Haki ya mtoto wa
miaka mitatu wa wanandoa hawa pia imekiukwa maana amelala bila kula kwa
siku ya leo ina maana Hakimu hana utu kiasi gani!!!!!
Nauomba uongozi wa Kituo cha
Sheria na Haki za Binadamu ulifuatilie kwa karibu suala hili kwani
Mhakama ni mahali patakatifu na ndipo kwenye chimbuko la Haki ya aina
yoyote,kama tunakuwa na Hakimu wa namna hii Haki itapatikana wapi!!!!!!
sikubaliani na vitendo vilivyofanywa na Hakimu huyu kwa vile vimetokana
na matakwa ya kujipatia fedha kwa njia ya Rushwa.
Taarifa hii imeandikwa na:
Antony Johnson Sollo
Mkurugenzi wa Shinyanga NguvuKazi Development Foundation SNDF
Kutoka Tinde Mkoani Shinyanga
+255 787 565 533/+255 713 565 533/+255 763 209 400
No comments: