Katibu Mkuu wa CCM Ndugu Abdulrahman Kinana akisalimiana na wakazi wa
kata ya Mwandoya ,kijiji cha Mandoya tarafa ya Kisesa ambapo Katibu Mkuu
alipata maelezo ya utekelezaji wa ilani ya CCM.
Katibu
Mkuu wa CCM Ndugu Abdulrahman Kinana akiangalia maendeleo ya hatua za
awali za ujenzi wa daraja la Mongobakama ambalo ni sehemu ya utekelezaji
wa ilani ya uchaguzi ya CCM.
Katibu
Mkuu wa CCM akipokelewa na umati wa wakazi wa kijiji cha Mwasengela
ambao kwa ni nadra kupata viongozi wa kitaifa kwenye kijiji chao.
Mkuu
wa Wilaya ya Meatu Rosemary Kirigini akisalimia wakazi wa kata ya
Mwasengela wakati wa mkutano wa hadhara ambao Katibu Mkuu wa CCM Ndugu
Abdulrahman Kinana alihutubia.
Mbunge
wa Kisesa Ndugu Luhaga Mpina akihutubia wakazi ya kata ya Mwasengela
kwenye mkutano wa hadhara ambao mgeni wa heshima alikuwa Katibu Mkuu wa
CCM Ndugu Abdulrahman Kinana.
Katibu
wa NEC Itikadi na Uenezi akihutubia wakazi wa kata ya Mwasengela ambapo
yupo kwenye ziara ya Katibu Mkuu wa CCM Ndugu Abdulrahman Kinana
mkoani Simiyu .
Katibu
Mkuu wa CCM Ndugu Abdulrahman Kinana akisalimiana na aliyekuwa mgombea
wa udiwani kwa tiketi ya TLP lakini sasa amejiunga rasmi na Chama Cha
Mapinduzi Zunzu Ndatulu kwenye mkutano wa hadhara uliofanyika
Mwasengela.
Katibu Mkuu wa CCM Ndugu Abdulrahaman Kinana akihutubia wakazi wa kata
ya Mwangesela wilayani Meatu mkoani Simiyu ambapo aliwasifu wakazi wa
kata hiyo kwa kuichagua CCM na kupata viongozi wanaoleta maendeleo.
:Mbunge wa Kisesa
Luhaga Mpina akiwatambulisha wazazi wake kwenye mkutano wa hadhara
ambapo aliwaambia wananchi ilimchukua miezi mitatu kukubaliwa kwa ombi
lake la kutaka kugombea ubunge jimboni kwake.
Chifu Kilabanja Abdulrahman Kinana akiwaaga wakazi wa kata ya Mwasengela baada ya kumaliza Mkutano wa hadhara.
Sehemu
ya umati uliofika kwenye mkutano wa hadhara kumsikiliza Katibu Mkuu wa
CCM Ndugu Abdulrahman Kinana, Katibu Mkuu yupo kwenye ziara ya mikoa
mitatu ambapo kwa sasa yupo mkoani Simiyu na atamalizia mkoa wa Mara,
tayari Katibu Mkuu ameshamaliza ziara ya mkoa wa Shinyanga na kuleta
neema kwa wakulima wa pamba na wafugaji.
Katibu
Mkuu wa CCM Ndugu Abdulrahman Kinana akiwa kwenye picha ya pamoja na
mbunge wa Kisesa Ndugu Luhaga Mpina na wazazi wa mbunge huyo mara baada
ya kumaliza mkutano wa hadhara.
Katibu Mkuu wa CCM Ndugu Abdulrahman Kinana amewataka mawaziri
husika kutatua kero za wananchi baada ya watendaji wa chini kushindwa
kufanya kazi zao, alisema sasa baadhi ya watendaji wamegeuza kero za
wananchi mitaji na kuwachajisha pesa nyingi hasa wafugaji.
Akihutubia
wakazi wa kata ya Mwasengela alisema mawaziri lazima wachukue jukumu la
moja kwa moja kutatua matatizo ya wananchi, alisema wafugaji wa kata ya
Mwasengela wamekuwa wakibughudhiwa na watu wa hifadhi ya Maswa kupita
kiasi, alisema sheria zingine ziangalia wakati zinaweza zikawa zimepitwa
na wakati hivyo ni vyema zikarekebishwa.
No comments: