Ads Top

Vijana wa Arsene Wenger watafungua pazia la Ligi ya Mabingwa leo kwa kuivaa Marseille nyumbani kwao


Kipa wa Marseille, Steve Mandanda amewatahadharisha Arsenal kuwa katika kundi la kifo walilopangwa wategemee kila mechi ni sawa na fainali
Gunners wanajua pamoja na kuwa na kiungo mpishi, Mesut Ozil na mshambuliaji Olivier Giroud, bado wanakabiliwa na ushindani mkali kutoka kwa Napoli na Borussia Dortmund katika kundi hilo.
Kipa huyo wa kimataifa wa Ufaransa, Mandanda alisema: “Mechi za makundi za Ligi ya Mabingwa ni ngumu. Kila klabu inataka kusonga mbele, hivyo mechi zote zinakuwa kama fainali na ni lazima ushinde nyumbani. Vinginevyo nafasi yako ya kusonga mbele itapotea.
“Giroud yupo katika kiwango kizuri. Tunatakiwa kuwazuia wasitufunge na kutokuwapa mwanya wa kucheza wanavyotaka, lakini hiyo haitokuwa kazi rahisi kwa sababu kwa sasa wana kikosi bora.
“Uwepo wa Ozil umeifanya safu ya ushambuliaji ya Arsenal kuwa hatari zaidi. Uwepo wake Arsenal na aina yake ya uchezaji ni ule anaoutaka Wenger. Sikutegemea Real Madrid watakubali kumwachia kirahi hivi aondoke.”
Madrid, Kocha wa Barcelona, Gerardo Martino atakiongoza kwa mara ya kwanza kikosi chake kucheza Ligi ya Mabingwa kwa kuwakaribisha Ajax Amsterdam kwenye Uwanja wa Nou Camp leo huku akisumbuliwa na ubutu wa safu yake ya ulinzi pamoja na ufungaji. Martino aliyerithi mikoba ya Tito Vilanova aliyewapa taji la nne la La Liga ndani ya misimu mitano iliyopita, lakini wakiwa na kumbukumbu ya kunyukwa mabao 7-0 na Bayern Munich katika mechi mbili za nusu fainali ya michuano hiyo.
Macho ya mashabiki wa Barca leo yatakuwa kwa Neymar na Lionel Messi ambao wameanza kuonyesha uelewano mzuri katika uchezaji wao.
Kocha wa Ajax, Frank de Boer, si mgeni machoni mwa mashabiki wa Barca kwani alishawahi kuichezea timu hiyo kati ya mwaka 1999 na 2003 na kutwaa taji la Ligi ya Hispania 1999 akiwa na pacha wake Ronald.
De Boer alisema kama Ajax watafanikiwa kupata pointi yoyote Barcelona itakuwa ni mafanikio makubwa kwao.
Mechi nyingine ya Kundi H inayochezwa leo ni AC Milan dhidi ya Celtic

No comments:

UHURUTZ. Theme images by hanoded. Powered by Blogger.