Ads Top

Waziri Mkuu Mstaafu na Mbunge wa Monduli Edward Lowassa Asimikwa Rasmi Kuwa Chifu wa Unyenyembe Mkoani Tabora

Waziri Mkuu Mstaafu na Mbunge wa Jimbo la Monduli,Mh. Edward Lowassa akivishwa vazi maalum la Kichifu pamoja na kukabidhiwa Mkuki na Chifu Mkuu wa Kabila la Unyenyembe,Chifu Msagata Fundikira ikiwa ni ishara ya kumsimika kuwa Chifu wa Kabila hilo,wakati wa Sherehe za Maadhimisho ya Kumbukumbu ya Mtemi Isike Mwanakiyungi aliefariki Miaka 124 iliyopita.Sherehe hizo zimefanyika jana kwenye Kijiji cha Itetemya,Mkoani Tabora.

Waziri Mkuu Mstaafu na Mbunge wa Jimbo la Monduli,Mh. Edward Lowassa  akionyeshwa moja ya kibuyu cha tambiko la wanyamwezi
Chifu mkuu wa unyanyembe,Chifu Msagata Fundikira akifanya tambiko muda mfupi baada kumtawaza Waziri Mkuu Mstaafu na Mbunge wa Jimbo la Monduli,Mh. Edward Lowassa
  Waziri Mkuu Mstaafu na Mbunge wa Jimbo la Monduli,Mh. Edward Lowassa pamoja na Chifu Mkuu wa Kabila la Unyenyembe,Chifu Msagata Fundikira wakishirikiana kuweka jiwe la msingi katika eneo litakalojengwa Mnara wa kumuenzi Mtemi Isike Mwanakiyungi aliefariki Miaka 124 iliyopita.Sherehe hizo zimefanyika jana kwenye Kijiji cha Itetemya,Mkoani Tabora.
Waziri Mkuu Mstaafu na Mbunge wa Jimbo la Monduli,Mh. Edward Lowassa (kulia) akisikiliza kwa makini Wasifu wa Marehemu,Mtemi Isike Mwanakiyungi aliefariki Miaka 124 iliyopita.Wasifu huo Ulisomwa na Bw. Richard Mchembe.
Waziri Mkuu Mstaafu na Mbunge wa Jimbo la Monduli,Mh. Edward Lowassa pamoja na Chifu Mkuu wa Kabila la Unyenyembe,Chifu Msagata Fundikira wakiwa kwenye picha ya pamoja na Machifu kutoka mikoa mbali mbali hapa nchini walioshiriki kwenye Sherehe za Maadhimisho ya Kumbukumbu ya Mtemi Isike Mwanakiyungi aliefariki Miaka 124 iliyopita.Sherehe hizo zimefanyika jana kwenye Kijiji cha Itetemya,Mkoani Tabora

No comments:

UHURUTZ. Theme images by hanoded. Powered by Blogger.