MKUU WA MKOA WA RUKWA STELLA MANYANYA AMUWAKILISHA WAZIRI MKUU MIZENGO PINDA KATIKA HARAMBEE YA UJENZI WA KANISA LA MORAVIAN MJINI SUMBAWANGA NA KUCHANGISHA ZAIDI YA MIL. 58

Mkuu
wa Mkoa wa Rukwa Injinia Stella Manyanya akizungumza katika harambee ya
kuchangisha fedha za ujenzi wa kanisa la Moravian Tanzania mjini
Sumbawanga akimuwakilisha Waziri Mkuu wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania
Mhe. Mizengo Pinda aliyemteua kufanya hivyo baada ya yeye kukabiliwa na
majumu mengine ya kitaifa. Awali Waziri Mkuu aliafiki mualiko wa Kanisa
hilo katika kuongoza harambee hiyo ambayo imefanikiwa kupata zaidi
ya Tsh. Milioni 58 zikiwepo fedha taslim zaidi ya shilingi Milioni
47 na nyingine zikiwa ni ahadi. Zimekuwepo pia ahadi za mifuko 30 ya
Cement na mlango mmoja mkubwa wa kuingilia kanisani hapo.

Mkuu
wa Mkoa wa Rukwa Stella Manyanya akitoa neno la awali kabla ya zoezi
hilo la harambee kuanza ambapo aliwaomba waumini na wageni waliofika
katika hafla hiyo kutoa kwa moyo katika kuchangia kazi hiyo ya
Mungu. Kwa kuanzia alitoa ahadi ya Waziri Mkuu aliyoitoa ambayo ni
milioni tano (5) na yeye mwenyewe kuchangia milioni moja. Aliendeleza
harambee hiyo kwa kuwachangisha kwanza viongozi wa Serikali alioambatana
nao na kuendelea na taratibu zingine kwa mujibu wa ratiba.

Askofu
Mkuu Conerad Nguvumali wa Kanisa la Moravian Tanzania Jimbo la Rukwa
akitoa neno katika hafla hiyo ambayo aliwataka waumini wa kanisa hilo
kuchapa kazi kwa nguvu na kuepukana na uvivu ambao alisema ni ugonjwa
mkubwa kuliko hata gonjwa la ukimwi. Alikemea pia tabia ya watu wengi
kuwahusisha watu waliofanikiwa kwa jitihada zao wenyewe na imani za
"Freemason" au "Ufisadi".

Mkuu
wa Wilaya ya Sumbawanga Methew Sedoyyeka akizungumza katika harambee
hiyo baada ya kupewa fursa na Mkuu wa Mkoa wa Rukwa kutoa mchango wake,
aliahidi mchango wa laki tano na mlango mmoja mkubwa wa kuingilia
kanisani hapo.

Baadhi
ya viongozi wa Serikali waliohudhuria katika hafla hiyo, kulia ni
Mkurugenzi wa Manispaa ya Sumbawanga William Shimwela ambaye pia ni
mwanakamati wa ujenzi katika kanisa hilo, Katikati ni Mbunge wa Jimbo la
Sumbawanga Mjini Aeshi Hillal na nyuma yake ni Kamanda wa Polisi Mkoa
wa Rukwa Mwaruanda.

Mkuu wa Mkoa wa Rukwa Mhandisi Stella Manyanya akiendelea na zoezi la uchangishaji.

Baadhi
ya waumini wa kanisa la Moravian Sumbawanga wakimfagilia kwa shangwe
Mbunge wa Jimbo la Sumbawanga Mjini Aeshi Hillal aliyachangia Tsh.
Milioni kumi zikiwepo za kwake binafsi Mil. 7 na nyingine Mil. 3
kuchangiwa na wabunge wenzake.Picha na Na Hamza Temba - Ofisi ya Mkuu wa Mkoa Rukwa
No comments: