Oktoba 20, Jumapili watani wa jadi Simba na Yanga watashuka kwenye Uwanja wa Taifa huku kila mmoja akijivunia ubora wa kikosi chake
Oktoba 20, Jumapili watani wa jadi Simba na Yanga watashuka kwenye Uwanja wa Taifa huku kila mmoja akijivunia ubora wa kikosi chake.
Oktoba 20, Jumapili watani wa jadi Simba na Yanga watashuka kwenye Uwanja wa Taifa huku kila mmoja akijivunia ubora wa kikosi chake.
Pamoja na ubora wa timu hizo katika uchunguzi
uliofanywa na Gazeti la Mwananchi umebaini kuwa timu hizo zimekuwa
zikiruhusu mabao ya kufungwa katika vipindi wanavyofunga mabao yao.
Simba wenyewe ni bora zaidi katika kipindi cha
kwanza wakiwa wamefunga mabao mengi, huku watani zao Yanga wenyewe
wamefunga mabao yao mengi kuanzia dakika 45 mpaka 80.
Simba katika michezo minane waliyocheza wamefunga
mabao 17, kati yake mabao 11 wamefunga kipindi cha kwanza na saba
kipindi cha pili kuanzia dakika ya 51 hadi 90.
Katika mechi nane Simba ilizocheza, matokeo yao
yalikuwa hivi na dakika walizofunga mabao yao katika mabano: Simba 2- 2
Rhino ( dakika 8, 37), Simba 2 - 0 Mtibwa (67, 90), Simba 6-0 Mgambo (
4, 32, 41, 44, 66, 77), Simba 2 - 2 Mbeya City ( 27, 33), Simba1 - 0
Prisons ( 57), Simba 2 - 0 JKT Ruvu ( 24, 48), Simba 1 - 1 Ruvu Shooting
( 51) Simba 1 - 0 Oljoro ( 41).
Safu ya ulinzi ya Simba iko vizuri kidogo kuliko
ya Yanga kwani imefungwa mabao machache kuliko wapinzani wao, lakini
imeonyesha udhaifu wa kufungwa mabao mengi kipindi cha kwanza kwani
katika michezo minane iliyocheza mpaka sasa imeruhusu mabao matano,
manne kipindi cha kwanza na moja kipindi cha pili.
Mabao ambayo Simba imefungwa kipindi cha kwanza:
Simba 2 - 2 Rhino( dakika 25, 35), Simba 2 - 2 Mbeya City ( 36),
Simba1-1 Ruvu Shooting ( 9) wakati goli moja pekee walilofungwa kipindi
cha pili ilikuwa dhidi ya Mbeya City dakika ya 67.
Mabingwa watetezi Yanga msimu huu wameonekana kuwa
wazito katika kushambulia kipindi cha kwanza, lakini ni wazuri katika
kujilinda zaidi muda huo.
Katika michezo minane ambayo Yanga imecheza
imefunga mabao 15, tisa kati ya hayo imefunga kipindi cha pili na sita
imefunga kipindi cha kwanza.
Yanga wamekuwa bora zaidi hasa kuanzia dakika ya
45 mpaka ya 80 kwani katika dakika hizo wamefunga mabao manane wakati
magoli mengine wamefunga dakika ya 90 na machache kipindi cha kwanza.
Matokeo ya Yanga katika mechi nane ilizocheza na
dakika walizofunga mabao. Yanga 5 - 1 Ashanti ( 10, 48, 57, 74, 90) ,
Yanga1-1 Mbeya City( 71), Yanga 1-1 Prisons ( 42), Yanga 2-3 Azam (40,
65), Yanga 2 - 1 Kagera ( 4, 60), Yanga 1- 0 Ruvu (62), Yanga 2- 0
Mtibwa (6, 20), Yanga 1-1 Coastal (65).
Pamoja na kuonyesha kuwa Yanga ni wakali wa kupachika mabao
kipindi cha pili hata hivyo safu yao ya ulinzi imeonekana ni dhaifu hasa
kipindi hicho.
Kwani katika michezo minane iliyocheza, imeruhusu
mabao manane, mabao saba yamefungwa katika kipindi cha pili na bao moja
tu wamefungwa kipindi cha kwanza.
Katika hayo mabao manane waliyofungwa Yanga, saba
wamefungwa kuanzia dakika ya 49 mpaka 90 hivyo kuonyesha dhaifu katika
kulinda goli lake katika kipindi hicho.
Mabao waliyofungwa Yanga katika kipindi cha pili:
Yanga 5 - 1 Ashanti 1 ( 89), Yanga1-1 Mbeya City (49), Yanga 1 - 1
Prisons ( 76) , Yanga 1 - 1 Coastal ( 90), Yanga 2 - 3 Azam ( 69, 90) ,
Yanga 2 - 1 Kagera ( 49).
Mshambuliaji wa Azam, John Bocco pekee ndiye aliyefanikiwa kutikisa nyavu za Yanga katika kipindi cha kwanza hadi sasa.
Kocha wa Simba, Abdallah Kibadeni alishangazwa na
thathimini hiyo na kudai ni nzuri na kuahidi kuitumia katika maandalizi
yake dhidi ya mchezo na Yanga.
“Sijafuatilia sana, lakini nafikiri sisi tunafunga
katika vipindi vyote ni jambo zuri kama mmeweza kuona hilo kwani nalo
litakuwa msaada kwangu kujua mapungufu ya kikosi changu na hata udhaifu
wa wapinzani wetu ili tutakapokutana mambo yawe mazuri,” alisema
Kibadeni.
Naye kocha msaidizi wa Yanga, Fred Felix Minziro
alisema, anajua timu yake ipo vizuri hasa kipindi cha pili na kutafuta
mabao ya ushindi.
“Sisi tuko vizuri muda wote ingawa ni kweli mabao
mengi tumefunga kipindi cha pili, lakini nafikiri ukosefu wa umakini kwa
washambuliaji kipindi cha kwanza nalo tatizo.
“Pia, timu nyingi zinatukamia hasa kipindi cha
kwanza, sisi huwa tunawaacha wakichoka sasa kipindi cha pili ndiyo
tunawamaliza,” alisema Minziro.
No comments: