TFDA Yateketeza samaki waliooza jijini Da es salaam



TFDA
imeteketeza samaki waliooza aina ya vibua wenye thamani ya takriban tsh
11,475,000 mali ya kampuni ya Sais Boutique. Samaki hao walioingizwa
nchini kutokea nchi ya China walikamatwa na TFDA katika eneo la Tabata
Bima wakati wa ukaguzi wa bidhaa za chakula. Kufuatia ukaguzi huo
uliofanyika septemba 18, 2013 Samaki hao walibainika wakiwa wameoza na
hawafai kwa matumizi ya binadamu. Samaki aina ya vibua wamekuwa ni maarufu kuuzwa maeneo ya feri na maeneo mengine ya mjini.
Mmiliki
wa kampuni ya Sais ailifunguLliwa kesi yenye namba BUG/RB/1184/2013 kwa
kosa la kuhifadhi samaki ambao wameoza, kuhifadhi katika eneo ambalo
halijasajiliwa na kushindwa kutoa taarifa kwa wakaguzi wa tfda kuhusu
uwepo wa samaki mpakani ambapo mtuhumiwa amehukumiwa kulipa faini ya sh.
1000, 000 na kuharibu mzigo kwa gharama zake.
No comments: