Tuzo ya amani ya Nobel, mwaka huu imekwenda kwa shirika la kudhibiti silaha za kemikali duniani OPCW
Wakaguzi wa silaha za kemikali Syria
Shirika hilo kwa sasa linasimamia shughuli ya kuharibu silaha za
kemikali za Syria ambazi zilitumiwa kwa mauaji ya raia wa nchi hiyo
mjini Damascus mwezi Agosti.
Tangazo hili limetolewa mjini Oslo, Norway.
Kufuatia uamuzi huu, kamati ya Nobel nchini
Norway imetambua kazi ya shirika hilo ambalo linaendesha shughuli ya
kuharibu silaha za kemikali, kama sehemu ya azimio la kimataofa la
kuharibu silaha za kemikali ambalo limesemekana kufanikiwa sana duniani.
Shirika hilo la kuzuia matumizi ya silaha za
kemikali , pia husimamia azimio la silaha za kemikali duniani ambalo
limefanikiwa kuharibu asimilia 80 ya zana za kemikali duniani.
Syria inatarajiwa kuwa nchi ya 131 kutia saini azimio hilo.
Nchi hiyo inasemekana kuwa na idadi kubwa ya silaha za kemikali duniani.
Tuzo ya leo kwa OPCW itaonekana kama hatua ya
kutia moyo kwa shirika hilo kuendelea na kusaidia katika kutatua mgogoro
wa kisiasa unaoendelea Syria
Waakilishi wa shirika hilo wataalikwa kupokea
medali na tuzo ya dola milioni 1.2 za kimarekani wakati wa sherehe
zitakazofanyika mwezi Disemba.
Habari na BBCSwahili.com
Habari na BBCSwahili.com
No comments: