Kutoka IKULU: Rais Jakaya Kikwete Akagua na Kuzindua Miradi Mkoa Mpya wa Simiyu
Rais
Dkt.Jakaya Mrisho Kikwete akisalimiana na Bwana Saguda Kasili mlemavu
ambaye pia ni mtendaji wa kijiji cha Ng’wang’wali jana wakati aliposimama
kijijini hapo kuwasalimia wananchi wa eneo hilo
Rais
Dkt.Jakaya Mrisho Kikwete akipanda mti wa kumbukumbu katika eneo la Old
Maswa muda mfupi baada ya kuzindua ujenzi wa barabara ya kilometa ya
Bariadi-Lamadi 71.8 huko eneo la old Maswa, Mkoani Simiyu.
Msanii wa kundi la sanaa kutoka
Bariadi akicheza na nyoka aina ya Chatu wakati wa uzinduzi wa Ujenzi wa
Barabara ya Bariadi –Lamadi Jana
Rais
Dkt.Jakaya Mrisho Kikwete,Waziri wa Ujenzi John Pombe Magufuli(watatu
kushoto),Mbunge wa Bariadi Mhe. Andrew Chenge(kushoto)pamoja na
viongozi wengine wakifunua kitambaa kuashiria kuweka jiwe la msingi na
kuzindua ujenzi wa Barabara ya Bariadi-Lamadi yenye urefu wa kilometa
71.8 huko enelo la Old Maswa mkoa mpya wa Simiyu jana
Rais
Dkt.Jakaya Mrisho Kikwete akikata utepe kuzindua rasmi Mradi wa Umeme
katika kijiji cha Nkololo wilayani Bariadi, Mkoa wa Simiyu Jana.Weninge
katika picha kutoka kushoto ni Naibu Waziri wa Nishati na Madini Mh.
Steven Masele, Mbunge wa Bariadi Mhe.Andrew Chenge(wapili
kushoto),Paroko wa Nkololo Padri Paulo Fegan(wanne kushoto) na kulia ni
Mkuu wa Mkoa wa Simiyu Pascal Mabiti.
Rais Dkt.Jakaya Mrisho Kikwete akisalimiana na baadhi ya wananchi waliohudhuria ufunguzi wa Barabara ya Bariadi Lamadi jana.
Rais
Dkt.Jakaya Mrisho Kikwete, Waziri wa Ujenzi John Pombe Magufuli(pembeni
ya Rais kulia) pamoja na viongozi wengine akikata utepe kuashiria
kuzindua rasmi ujenzi wa Barbara ya Bariadi Lamadi yenye urefu wa
kilometa 71.8 huko eneo la Old Maswa jana.Picha na IKULU
No comments: