MAKAMU MWENYEKITI WA CCM NDUGU PHILIP MANGULA ZIARANI MKOANI RUKWA
Makamu Mwenyekiti wa Chama cha Mapinduzi
CCM Ndugu Philip Mangula akifurahia jambo na Katibu Tawala Mkoa wa
Rukwa Alhaj Salum Mohammed Chima mara baada ya kuwasili Mkoani Rukwa
akitokea Katavi kwa ziara ya kichama hivi karibuni. Mheshimiwa Mangula
atamaliza ziara yake leo tarehe 12 Novemba 2013 Mkoani Rukwa ambapo
amefanya mikutano mbalimbali ya nje na ya ndani pamoja na kukagua miradi
mbalimbali inayoendeshwa na Chama cha Mapinduzi na Serikali.
Makamu Mwenyekiti wa CCM Philip Mangula
akisalimiana na Mkuu wa Wilaya ya Nkasi Iddi Kimanta alipowasili
Wilayani hapo hivi karibuni kwa ziara ya kichama ya siku nne Mkoani
Rukwa.
Makamu Mwenyekiti wa CCM Philip Mangula
akipeana mikono na Mbunge wa Nkasi Kusini Ali Kessy maarufu kama Ali
Mabodi katika ziara yake Wilayani Nkasi hivi karibuni.
Makamu Mwenyekiti wa CCM Taifa watatu
kushoto, Mwenyekiti wa CCM Mkoa wa Rukwa Hiporatus Matete wa pili
kushoto na Katibu wa CCM Mkoa wa rukwa wakifurahia mapokezi ya wananchi
wa kijiji cha Kizi kilichopo Wilayani Nkasi waliokuwa wakimlaki Makamu
Mwenyekiti wa CCM Taifa Ndugu Philip Mangula kwa ujio wake Mkoani Rukwa.
Mkuu wa Mkoa wa Katavi Dkt. Rajab Mtumwa
Rutengwe wa pili kushoto na msafara wa viongozi wa Chama Tawala kutoka
Mkoa wa Katavi wakiondoka katika viwanja vya Kizi baada ya kumuaga
na kumkabidhi Makamu Mwenyekiti wa CCM Philip Mangula kwa viongozi wa
Chama na Serikali Mkoa wa Rukwa kwa ajili ya ziara ya kichama Mkoani
humo.
No comments: