Kutoka Chama Cha Mapinduzi(CCM):Katibu Mkuu wa CCM Ndugu Abdulrahaman Kinana ataanza ziara ya siku 22 kwenye mikoa ya Ruvuma na Mbeya kuanzia tarehe 15/11/2013 mpaka mwanzoni mwa mwezi wa Desemba 2013.
Katibu wa Halmashauri Kuu ya Taifa Itikadi na Uenezi Nape Nnauye
Katibu Mkuu wa CCM Ndugu Abdulrahaman Kinana ataanza ziara ya siku 22 kwenye
mikoa ya Ruvuma na Mbeya kuanzia tarehe 15/11/2013 mpaka mwanzoni mwa mwezi wa
Desemba 2013. Huu ni mwendelezo wa ziara za kichama katika kuimarisha chama, kukagua
utekelezaji wa Ilani ya Uchaguzi ya CCM ya mwaka 2010, kusikiliza kero mbalimbali za wananchi na
kushirikiana nao kuzitafutia ufumbuzi.
Katika ziara zilizopita na vikao kadhaa vya chama Serikali iliagizwa
kushughulikia baadhi ya kero, na tumeshuhudia baadhi ya hoja hizo zikichukuliwa
hatua. Baadhi ya hoja zilizoanza kushughulikiwa na Serikali ni pamoja na:-
1) Hoja
ya kufufua viwanda nchini.
Baada ya ziara kadhaa za Katibu Mkuu, uchambuzi na vikao kadhaa vya CCM, Chama kiligundua kuwa viwanda vingi vilivyo binafsishwa havifanyi kazi kama ilivyokusudiwa na vingine kufungwa kabisa na kugeuzwa magodauni.

Pamoja na athari kubwa kwa uchumi wa nchi yetu, kufungwa na kutofanya vizuri
kwa viwanda hivyo kumechangia sana tatizo la ajira nchini kuwa kubwa. Hivyo
Chama kiliagiza Serikali kufanya tathmini ya viwanda vyote vilivyo binafsishwa
na hali yake kwa sasa na vile visivyofanya kazi kama ilivyokusudiwa vichukuliwe
na Serikali na kutafuta njia sahihi ya kuvifufua upya.
Serikali imechukua hatua kadhaa katika hili, ikiwemo kufanya tathmini na mapendekezo kadhaa yamewasilishwa na timu iliyoundwa na Serikali kwa ajili ya kufanyia uamuzi na kuchukua hatua.
Serikali imechukua hatua kadhaa katika hili, ikiwemo kufanya tathmini na mapendekezo kadhaa yamewasilishwa na timu iliyoundwa na Serikali kwa ajili ya kufanyia uamuzi na kuchukua hatua.
Tunajua
zipo hatua kadhaa zimechukuliwa katika jitihada za kufufua viwanda vya kubangua
korosho kama sehemu ya utatuzi wa tatizo la soko na zao la korosho. Pia Serikali
ipo katika hatua kadhaa za kushughulikia viwanda vingine nchini.
Tunaipongeza serikali kwa hatua hii muhimu ya kutekeleza agizo la chama.
Tunaitaka serikali ikamilishe zoezi hili mapema iwezekanavyo ili nchi ifaidike
na ufufuaji huu wa viwanda nchini.
2) Changamoto kwa wakulima wa pamba
Katika ziara ya Katibu Mkuu mikoa kadhaa ya Kanda ya Ziwa, alitumia muda mrefu
kujifunza na kuzungumza na wakulima wa zao la pamba wa mikoa hiyo. Pamoja na
tatizo kubwa la soko na bei ya pamba, pamekuwa na changamoto kubwa ya
mfumo unaosimamia zao la pamba ikiwemo upatikanaji wa pembejeo.
Hatua
kadhaa zimeanza kuchukuliwa na Serikali ikiwa ni pamoja na kuvutia uwekezaji
kwenye viwanda vya kutengeneza nyuzi, nguo na kukamua mafuta ya pamba.
Tulishuhudia ujenzi wa viwanda kadhaa mjini Shinyanga, vingi vikijengwa na
wawekezaji kutoka China.
Lakini wakati wa Bunge la juzi, Serikali imeamua kutoa ruzuku ya asilimia hamsini kwa mbegu bora za pamba ili kuwawezesha wakulima kumudu bei ya mbegu hizo na hivyo kuboresha zao la pamba nchini na maisha ya wakulima kuwa bora zaidi.(bei ya dukani kwa kilo moja ni Sh. 1,200/=; Serikali italipia

Sh.600/=).
Katika hili la mbegu bora na kilimo cha mkataba tunaitaka Serikali na hasa wakuu wa wilaya na mkoa kuacha mara moja kutumia nguvu kuwalazimisha wakulima kulima kwa mkataba na kutumia mbegu bora badala yake wawaelimishe na kuwashawishi badala ya kutumia nguvu.

Tunaipongeza Serikali kwa kuanza kuchukua hatua za kutekeleza baadhi ya
mapendekezo ya CCM ya namna ya kutatua matatizo yanayowakabili wakulima wa
pamba nchini. Tunaitaka Serikali kuongeza kasi ya utatuaji wa changamoto hizo
ili wakulima wa pamba wafaidike na uchumi wa nchi kukua kwa kasi nzuri.
3). Migogoro
kati ya wakulima, wafugaji na hifadhi juu ya matumizi ya
ardhi
Katika ziara mbalimbali za Katibu Mkuu kwenye mikoa kama ya Morogoro, Njombe, Simiyu, Mara n.k. alishuhudia migogoro mingi sana juu ya wakulima, wafugaji na hifadhi mbalimbali nchini. Hakuna shaka migogoro hiyo imegharimu sana maisha ya watu na mali zao na hata uchumi wa nchi yetu.

Chama
kiliagiza migogoro hiyo kushughulikiwa mapema na kupata ufumbuzi wa kudumu.
Chama kinalipongeza Bunge na hasa Wabunge wa CCM na Serikali yake kwa uamuzi wa
kuunda Kamati teule ya Bunge kuchunguza na kutoa
mapendekezo
ya hatua kadhaa za kuchukuliwa katika kufikia suluhisho la kudumu kwa migogoro
hii.
Tunawaomba wananchi watoe ushirikiano wa kutosha kwa kamati teule ya Bunge ili
kazi hii ya kamati iwe na matokeo mazuri yatakayosaidia kumaliza tatizo hili nchini.
Wakati Kamati teule ya Bunge ikifanya kazi yake, tunawaomba wakulima na
wafugaji kote nchini kutulia kusubiri matokeo ya kamati hii teule ya Bunge.
Hivyo
basi, ziara hii ya Katibu Mkuu imelenga
pamoja na mambo mengine kuimarisha Chama, kukagua Ilani ya Uchaguzi ya CCM na
kusikiliza kero za wananchi. Tumeona jinsi ziara zilizotangulia zilivyokuwa na
matokeo mazuri, tunaamini ziara hii pia itakua na matokeo mazuri.
Imetolewa na:-
Imetolewa na:-
(Sgd.)
Nape Moses Nnauye,
KATIBU WA HALMASHAURI KUU YA TAIFA
Nape Moses Nnauye,
KATIBU WA HALMASHAURI KUU YA TAIFA
ITIKADI NA UENEZI
12/11/2013
No comments: