Shughuli ya kutia saini mkataba wa amani kati ya waasi wa M23 na serikali ya Jamhuri ya kidemokrasia ya Congo, iliyokukuwa imepangwa kufanyika Jumatatu , iligonga mwamba
Hii ni kutokana na serikali ya Congo kusema kuwa mkataba huo uangaliwe upya na hivyo kulazimisha shughuli hiyo kuahirishwa.
Mpatanishi wa pande hizo mbili
Ofuono Opondo wa Uganda, alisema kuwa pande hizo hazikuwa tayari kuonana
ana kwa ana baada ya DRC kusema kuwa M23 watie saini mkataba katika
chumba tofauti na kisha wapewe wao kuusaini.
Hata hivyo mpatanishi alisema haiwezekeni kwa
hilo kufanyika kwa sababu pande zinazozozana lazima zikae katika chumba
kimoja kwa ajili ya kufanikisha juhudi za upatanishi.
Kundi la waasi la M23 lilisitisha uasi wao baada
ya kupata kipigo kutoka kwa wanajeshi wa DRC wakisaidiwa na wanajeshi
wa Umoja wa Mataifa waliowafurusha kutoka maficho yao ya milimani katika
mpaka wa Rwanda na Uganda.
Mkataba huo ulistahili kutiwa saini mjini Kampala Uganda, ingawa shughuli yenyewe ilicheleweshwa bila ya kujua itafanyika lini.
Ali Mutasa
anasema kuwa mpatanishi mkuu Ofwono Opondo alisema mkataba hautatiwa
saini na kwamba haijulikani ni lini makubaliano hayo yatasainiwa.
Alisema Upande wa M23 uko tayari kwa shughuli hiyo na kuwa kizungumkuti
kimetokana upande wa DRC.
Serikali ya DRC kupitia kwa msemaji wake,Lambert
Mende ilisema kuwa Kinshasa iko tayari kutia saini makubaliano hayo,
lakini sio mkataba unaosema ni makubaliano ya amani kwa sababu ni kama
kundi hilo bado lipo.
Duru zinasema kuwa Rais Yoweri Museveni pamoja
na wanadiplomasia wa nchi za Magharibi, walisburi mkataba kutiwa saini
lakini wajumbe wa DRC hawakuingia katika chumba cha hafla hiyo ya kutia
saini.
No comments: