MAAFA MAKUBWA YATOKEA UFILIPINO KUFUATIA KUKUMBWA NA KIMBUNGA HAIYAN
Madhara ya kimbunga Haiyan Ufilipino
Marekani imepeleka ndege na meli za mizigo kwenda Ufilipino, wakati ambapo Uingereza imepeleka meli ya kivita.
Watu wapatao 10,000 wanahofiwa kufa, na maelfu ya walionusurika katika kimbunga Haiyan wanahitaji msaada.
Rais wa Ufilipino Benigno Aquino ametangaza hali hiyo kuwa janga la kitaifa.
Katika taarifa yake, Rais Aquino,amesema majimbo
mawili ya Leyte na Samar yameathirika zaidi kutokana na kimbunga hicho,
ikiwemo watu wengi kupoteza maisha.
Juhudi kubwa za kimataifa zinafanyika ili kutoa
msaada wa dharura kwa Ufilipino, lakini wafanyakazi wa mashirika ya
kutoa msaada wanakwama kuyafikia maeneo yaliyokumbwa na kimbunga.
Katibu Mkuu wa Umoja wa Mataifa, Ban Ki-moon
amezielezea picha zinazoonyesha ya kimbunga hicho kuwa zinatisha na
kukatisha tamaa.
Umoja wa Mataifa utazindua mpango mkubwa wa
msaada wa kibinadamu, na kutenga dola milioni 25 kusaidia jitihada za
misaada ya dharura.
"Maelfu ya watu wameripotiwa kufa na watu
wapatao milioni kumi wameathirika kutokana na kimbunga hicho. Hebu
tuonyeshe mshikamano wetu na watu wa Ufilipino katika kipindi hiki cha
kuhitaji msaada," amesema.
Habari na BBCSwahili.com
Habari na BBCSwahili.com
No comments: