Shehena kubwa ya pembe za tembo ikiwa na vipande 1,021 na uzito wa kilo 2,915 ambayo haijawahi kukamatwa nchini imenaswa katika bandari ya Zanzibar huku ikishuhudiwa na mawaziri wa serikali zote mbili wakiongozwa na waziri wa mali asili na utalii Mhe Khamis Kagasheki.
Baadhi
ya Pembe za Tembo zilizokamatwa katika bandari ya Malindi Zanzibar
yakisubiri kuhisabiwa kupata idadi kamali na thamani yake na uzito kwa
ujumla.
Zoezi likiendelea kupekuwa makunia ya Makombe ya Pwani kutowa magunia yaliohifadhiwa Pembe za Tembo
Askari
wa jeshi la Polisi wakitowa Pembe za Tembo katika makunia wakati wa
zoezi hilo leo asubuhi katika bandari ya Malindi Zanzibar.
Zikipimwa uzito kujuwa uzito wake kila gunia likipimwa kupata uzito wake wote.
Operesheni
Ikiendelea kuhesabu Pembe za Tembo zilizokamatwa katika bandari ya
Zanzibar wakiweka hesabu sawa kuhakikisha hesabu iliokamilika na kupata
thamani yake halithi.
Kamanda
wa Kikosi cha Polisi Bandarini Zanzibar akiongoza Operesheni wa kukagua
magunia yaliokuwa na Pembe za Tembo yaliokamatwa katika bandari hiyo
leo yakiwa katika harakati ya kusafirishwa nje ya Nchi kupitia bandari
hiyo, zoezi hilo limefanywa chini ya Jeshi la Polisi Bandari Kikosi cha
KMKM, yalikuwa katika Kontena la futi 40.
Magunia
haya yakiwa na sehena na makombe ya pwani wakati katikati yakiwa na
viroba vya mPembe za Tembo ambayo yakiwa yamehifadhiwa katika Kontena
likiwa tayari kusafirishwa nje ya Nchi, limegunduliwa katika bandari ya
Zanzibar jana asubuhi
No comments: