WAZIRI DK.NCHIMBI AZINDUA MPANGO MKAKATI WA MIAKA MITATU WA KUBORESHA MADAWATI YA KIJINSIA NA WATOTO NDANI YA JESHI LA POLISI
Mratibu Mkazi wa Umoja wa Mataifa nchini Dr. Alberic Kacou akisalimiana
na Kamanda wa Kanda Maalum Dsm, Kamishina Msaidizi wa Jeshi la Polisi
(ACP) Suleiman Kova alipowasili kwenye uzinduzi wa Mpango Mkakati wa
miaka mitatu wa Kuboresha Madawati ya Kijinsia na Watoto ndani ya Jeshi
la Polisi. Tukio hilo lilifanyika Kituo cha Polisi Chang’ombe, Temeke
jijini Dar es Salaam.
Mratibu Mkazi wa Umoja wa Mataifa nchini Dr. Alberic Kacou
akibadilishana mawazo na Mkuu wa Jeshi la Polisi nchini (IGP) Said
Mwema.Kulia ni Kamanda wa Kanda Maalum Dsm, Kamishina Msaidizi wa Jeshi
la Polisi (ACP) Suleiman Kova. Kushoto ni Wanamawasiliano kutoka Ofisi
ya Mratibu Mkazi wa Umoja wa Mataifa Hoyce Temu na Sangita Khadka.
Mkuu
wa Jeshi la Polisi nchini (IGP) Said Mwema akimtambulisha mgeni rasmi
Waziri wa Mambo ya Ndani ya Nchi, Dk. Emmanuel Nchimbi kwa baadhi ya
maafisa wa Jeshi la Polisi nchini mara baada ya kuwasilia eneo la tukio.
Mgeni
rasmi Waziri wa Mambo ya Ndani ya Nchi, Dk. Emmanuel Nchimbi
akibadilishana mawazo na Mkuu wa Jeshi la Polisi nchini (IGP) Said Mwema
(kushoto) na Kulia ni Kamanda wa Kanda Maalum Dsm, Kamishina Msaidizi
wa Jeshi la Polisi (ACP) Suleiman Kova wakati wakielekea jukwaa kuu.
Balozi wa Ireland nchini Fionnuala Gilsenan (katikati) akiteta jambo na
Mratibu Mkazi wa Umoja wa Mataifa nchini Dr. Alberic Kacou (kushoto)
Kulia ni Mkuu wa Mabalozi wa EU nchini Filiberto Sebregondi.
Pichani juu na chini Maandamano yakiwasili kwenye uzinduzi wa Mpango
Mkakati wa miaka mitatu wa Kuboresha Madawati ya Kijinsia na Watoto
ndani ya Jeshi la Polisi.
Taasisi mbambali zikiwa zimebeba mabango yenye jumbe mbalimbali za kutokomeza ukatili wa Kijinsia.
Meza Kuu ikipokea maandamano.
Burudani kwenye uzinduzi wa Mpango Mkakati wa miaka mitatu wa Kuboresha
Madawati ya Kijinsia na Watoto ndani ya Jeshi la Polisi.
Waziri wa Mambo ya Ndani ya Nchi, Dk Emmanuel Nchimbi akitoa hotuba
yake kwa Askari na Maofisa wa Jeshi la Polisi, Viongozi wa Mashirika na
Taasisi zisizo za Serikali pamoja na wakazi wa Temeke kabla ya kuzindua
Mpango Mkakati wa miaka mitatu wa Kuboresha Madawati ya Kijinsia na
Watoto ndani ya Jeshi la Polisi. Tukio hilo lilifanyika Kituo cha Polisi
Chang’ombe, Temeke jijini Dar es Salaam leo. Kulia ni Waziri Nchimbi
akatika hotuba yake alilishukuru Jeshi la Polisi pamoja na Viongozi wa
Mashirika na Taasisi zisizo za Serikali kwa kusaidia masuala ya
kupambana na unyanyasaji wa kijinsia nchini.
Mratibu Mkazi wa Umoja wa Mataifa nchini Dr. Alberic Kacou
Mkuu wa Jeshi la Polisi nchini (IGP) Said Mwema akizungumza kwenye uzinduzi wa Mpango Mkakati wa miaka mitatu wa Kuboresha Madawati ya Kijinsia na Watoto ndani ya Jeshi la Polisi.
Balozi wa Umoja wa Ulaya nchini, Balozi Filiberto Ceriani Sebregondi akizungumza kwenye hafla hiyo.
Balozi wa Ireland nchini Fionnuala Gilsenan akizungumza kwa niaba ya
nchi yake ambapo amesema Ireland itaendelea kushirikiana na Serikali ya
Tanzania kwa ukaribu zaidi.
Waziri wa Mambo ya Ndani ya Nchi, Dk Emmanuel Nchimbi akizindua kitabu
cha Mpango Mkakati wa miaka mitatu wa kuboresha madawati ya Kijinsia na
Watoto ndani ya Jeshi la Polisi katika uzinduzi uliofanyika Kituo cha
Polisi Chang’ombe, Temeke jijini Dar es Salaam. Kulia ni Mkuu wa Jeshi
la Polisi nchini (IGP) Said Mwema, wa pili kulia ni Mratibu Mkazi wa
Umoja wa Mataifa nchini Dr. Alberic Kacou, wapili kushoto ni Balozi wa
Umoja wa Ulaya nchini, Balozi Filiberto Ceriani Sebregondi na Kushoto ni
Kamanda wa Polisi, Kanda Maalumu ya Dar es Salaam, Suleiman Kova.
Waziri Nchimbi akatika hotuba yake alilishukuru Jeshi la Polisi pamoja
na Viongozi wa Mashirika na Taasisi zisizo za Serikali kwa kusaidia
masuala ya kupambana na unyanyasaji wa kijinsia nchini
Waziri wa Mambo ya Ndani ya Nchi, Dk Emmanuel Nchimbi akikionyesha
kitabu cha Mpango Mkakati wa miaka mitatu wa kuboresha madawati ya
Kijinsia na Watoto ndani ya Jeshi la Polisi katika uzinduzi uliofanyika
Kituo cha Polisi Chang’ombe, Temeke jijini Dar es Salaam.
Waziri wa Mambo ya Ndani ya Nchi, Dk Emmanuel Nchimbi akimshukuru
Mratibu Mkazi wa Umoja wa Mataifa Dr. Alberic Kacou mara baada ya
kuzindua Mpango Mkakati wa miaka mitatu wa kuboresha madawati ya
Kijinsia na Watoto ndani ya Jeshi la Polisi ulio chini ya Umoja wa
Mataifa.
Waziri wa Mambo ya Ndani ya Nchi, Dk Emmanuel Nchimbi akikata utepe
kuzindua ofisi ya Dawati la Jinsia na Watoto katika Mkoa wa Kipolisi
Temeke. Kushoto ni Balozi wa Umoja wa Ulaya nchini, Balozi Filiberto
Ceriani Sebregondi.Waziri Nchimbi katika hotuba yake alilishukuru Jeshi
la Polisi pamoja na Viongozi wa Mashirika na Taasisi zisizo za Serikali
kwa kusaidia masuala ya kupambana na unyanyasaji wa kijinsia nchini.
Sasa imezinduliwa rasmi.
Waziri wa Mambo ya Ndani ya Nchi, Dk Emmanuel Nchimbi (wa tatu kulia)
akiwa katika picha ya pamoja na maofisa wa Jeshi la Polisi pamoja na
Viongozi wa Mashirika na Taasisi zisizo za Serikali baada ya waziri huyo
kuzindua Mpango Mkakati wa miaka mitatu wa Kuboresha Madawati ya
Kijinsia na Watoto ndani ya Jeshi la Polisi. Tukio hilo lilifanyika
Kituo cha Polisi Chang’ombe, Temeke jijini Dar es Salaam leo. Wapili
kulia ni Mkuu wa Jeshi la Polisi nchini (IGP) Said Mwema.
Mratibu Mkazi wa Umoja wa Mataifa Dr. Alberic Kacou akiteta jambo na
mmoja wa maafisa wa Jeshi la Polisi mara baada ya uzinduzi huo.
Mratibu Mkazi wa Umoja wa Mataifa Dr. Alberic Kacou akifanya mahojiano
na mwandishi wa habari wa redio wa BBC. Katikati ni Afisa Habari wa
kitengo cha Habari cha Umoja wa Mataifa Usia Nkhoma Ledama.
Waziri wa Mambo ya Ndani ya Nchi, Dk Emmanuel Nchimbi akiagana na
Mratibu Mkazi wa Umoja wa Mataifa Nchini, Dr. Alberic Kacou mara ya
uzinduzi.
No comments: