Taarifa Kwa Umma Kutoka Ofisi ya Waziri Mkuu: WAZIRI MKUU Mizengo Pinda amesema anatamani kuona Serikali za Mitaa hapa nchini zinasimamia maendeleo kuanzia ngazi ya chini kwa kushirikiana na sekta binafsi ikiwa ni njia ya kuharakisha maendeleo kwa wananchi.
Waziri Mkuu Mizengo Pinda
JAMHURI YA MUUNGANO WA TANZANIA
OFISI YA WAZIRI MKUU
WAZIRI
MKUU Mizengo Pinda amesema anatamani kuona Serikali za Mitaa hapa
nchini zinasimamia maendeleo kuanzia ngazi ya chini kwa kushirikiana na
sekta binafsi ikiwa ni njia ya kuharakisha maendeleo kwa wananchi
Ametoa kauli hiyo huo jana mchana (Jumatatu, Novemba 25, 2013) wakati
akizungumza na waandishi wa habari mara baada ya kufungua mkutano wa
ushirikiano baina ya Mamlaka za Serikali za Mitaa za China na Tanzania
ulioanza leo jijini Dar es Salaam.
“Ni
muhimu tukaanzisha ushirikiano huu kwenye ngazi ya Serikali za Mitaa
kwa sababu usimamizi wake unakuwa karibu zaidi na wananchi kuliko ilivyo
hivi sasa”, alisema.
Kuhusu
ujio wa magavana, mameya na wafanyabiashara wapatao 71 kutoka majimbo
manne ya Shandong, Liaoning, Shaanxi na Jilin, Waziri Mkuu alisema ujio
wao umekuja wakati muafaka kwani unasaidia kujenga mahusiano ya karibu
zaidi na wananchi kwenye ngazi ya chini kuliko inavyokuwa kuna mahusiano
kwenye ngazi ya Kitaifa peke yake.
“Hawa
waliokuja wanatoka majimbo manne tu kati ya majimbo 31 ya nchi hiyo,
tungependa kila mwaka tupate wajumbe wa aina tofauti hadi tufikishe
majimbo 15 au 20 hivi… tunataka ushirikiano huu ukue zaidi uende hadi
katika miji mikubwa ya Beijing ama Shanghai,” aliongeza.
Katika
hotuba yake kwa wajumbe wa mkutano huo, Waziri Mkuu aliwataka watumie
fursa hiyo kubadilishana uzoefu na kufanikisha mahusiano ya kibishara si
tu baina yao, bali hata katika ngazi ya Halmashauri wanazotoka baadhi
ya wajumbe.
Mapema
akizungumza na washiriki wa mkutano huo, Balozi wa China nchini
Tanzania, Dk. Lu Youqing alisema biashara kati aya China na Tanzania
imeongezeka na kufikia Dola za Marekani bilioni 2.47 ambalo ni ongezeko
la asilimia 15.2 ikilinganishwa na hali ilivyokuwa mwaka jana.
Alisema
hadi kufikia Juni, 2013, makampuni zaidi ya 500 kutoka China yalikuwa
yamekwishasajiliwa hapa nchini yakiwa na mtaji wa Dola za Marekani
bilioni 2.175 na kuifanya China iwe ni mwekezaji wa pili kwa ukubwa hapa
nchini Tanzania.
Naye
Naibu Gavana wa Jimbo la Shandong, Bw. Xia Geng ambaye pia ni kiongozi
wa msafara huo, alisema Agosti, 2013 China ilileta madaktari 23 wa fani
tofauti ili kusaidia kujenga kada ya watalaam wa sekta ya afya hapa
nchini.
Alisema
maeneo makuu ambayo wamelenga kuyazingatia katika ziara yao hii ni
Kilimo; Nishati; Utunzaji wa Mazingira na uchimbaji wa rasilmali za
ardhini.
Alisema
ifikapo mwaka 2014, wakati Tanzania na China zinatarajiwa kuadhimisha
miaka 50 ya urafiki baina yao, angependa kuona maeneo hayo ya msingi
yakiwa yamepewa kipaumbele katika utekelezaji wake.
Mkutano
huo umehudhuriwa pia na Waziri wa Nchi (OWM-TAMISEMI), Bibi Hawa
Ghasia; Waziri wa Nchi Ofisi ya Rais (Asiyekuwa na Wizara Maalum), Prof.
Mark Mwandosya, Wakuu wa mikoa 25, Makatibu Tawala wa Mikoa 25, Wakuu
wa Wilaya 50, Wakurugenzi wa Halmashauri 95 na wafanyabiashara kadhaa.
IMETOLEWA NA:
OFISI YA WAZIRI MKUU,
S. L. P. 3021,
DAR ES SALAAM.
JUMATATU, NOVEMBA 25, 2013
No comments: