Ajali ya Ngema lilokatika na Kusababisha Vifo Vya Watu Sita na Kujeruhii Watatu katika machimbo ya Pumwani, wilaya ya Moshi vijijini, mkoani Kilimanjaro.
“Hili ni pigo kubwa sana, poleni sana kwa janga hili
lililowakuta, na ninatoa agizo kwamba ni marufuku kuendelea na shughuli za
uchimbaji, Mkuu wa wilaya simamia hili na kuhakikisha Machimbo haya yanafungwa
kuanzia sasa, tayari nimeshawasiliana na wataalamu wa Madini kutoka Arusha,
kuja kukagua na kutathmini athari ambazo zinaweza kujitokeza tena”, alisema
Gama.
Aidha watu watatu waliyojeruhiwa katika Maporomoko hayo
ni pamoja na Dereva wa gari lililokuwa likipakiza mchanga katika Machimbo hayo
wakati wa tukio, Antipus Babu (56), ambaye alipata majeraha kichwani na
amelazwa katika Hopitali ya Rufaa ya KCMC.
Watu wengine waliopoteza Maisha katika tukio hilo la
pili kutokea kwenye machimbo hayo, katika kipindi cha Mwaka mmoja, ni Efrahim Assei
(27), Mkazi wa Kawawa, Ludovick Venance (16), mkazi wa Pumwani, Omari Masoud
(33), mkazi wa Pumwani na August Lyimo (26), Mkazi wa Pumwani.
Katika zoezi hilo lilichukua takribani masaa sita,
miili ya watu sita iliondolewa katika Kifusi hicho, ikiwemo maiti ya wanafunzi
wawili, David Macha (18), ambaye ni Mwanafunzi wa kidato cha pili, katika shule
ya Sekondari ya Ebenezer-Sango, aliyekuwa anafanya kibarua kama mchimbaji
katika Machimbo hayo na Marwa Mwita (14), ambaye alimaliza Darasa la Saba Mwaka
huu, na kuchaguliwa kujiung ana shule ya Sekondari Uparo.
Wengine ni Utingo wa gari hilo, Simon Mosha (21),
ambaye alipata majeraha kidogo na kutibiwa papo hapo katika eneo la tukio
pamoja na Mtu mmoja aliyejulikana kwa jina moja la Charles (30), mkazi wa
Sango, ambaye anaripotiwa kuwa katika hali mbaya na amelazwa katika chumba cha
ungalizi wa Madaktari (ICU), katika Hopitali ya KCMC.
Gama alisema pamoja na agizo hilo, tayari uongozi wa
Mkoa umeshawasiliana na Wataalam wa Madini wa Kanda, kutoka MKoani Arusha
kufika katika eneo hilo na kufanya ukaguzi wa kitaalam kabla ya kuruhusu zoezi
la uchimbaji kuendelea.
Akizungumza na Mamia ya Wananchi waliofika katika eneo
hilo, kushiriki zoezi la uokoaji, Mkuu wa Mkoa wa huo, Leonidas Gama aliagiza
kusitishwa kwa shughuli za uchimbaji katika Machimbo hayo pamoja na Machombo
mengine Mkoania hapo, ikiwemo lile lililopo katika eneo la Uchira ambayo
inasemekana kuwa katika hali mbaya.
Sehemu ya Miili iliyotolewa
Kamanda wa Polisi Mkoa wa Kilimanjaro Robert Boaz,
aliwataka wachimbaji katika Machimbo yote kuwa makini hasa katika kipindi hiki
cha mvua kwani udongo sasa hivi unaingia maji kwa hiyo uwezekano wa kukatika na
kusababisha maafa ni makubwa sana.
Kamanda Boaz alisema miili ya Marehemu imehifadhiwa
katika Hopitali ya Rufaa ya Mkoa wa Kilimanjaro (MAWENZI) na kwamba juhudi za
kuhakikisha uhai wa waliojeruhiwa unaokolewa zinaendelea.
WATU Sita wamepoteza Maisha na wengine watatu
wakijeruhiwa vibaya baada ya Ngema kukatika na kuwafukia wakiwa wanachimba
mchanga katika machimbo ya Pumwani, wilaya ya Moshi vijijini, mkoani
Kilimanjaro.
Mara baada ya kutokea kwa tukio hilo, wananchi
wakishirkiana na timu nzima ya ulinzi na usalama wa Mkoa, wakiongozwa na Mkuu
wa Mkoa wa Kilimanjaro, Leonidas Gama
walifika katika eneo la tukio na kuanza juhudi za kuwafukua wahanga hao.
Watu hao ambao ni wachimbaji, walikutwa na masaibu
hayo jana majira ya saa 10:30 alasiri, wakati wakiwemo wanafunzi wawili,
walikutwa na masaibu hayo wakati wakiwa wanapakiza mchanga kwenye gari aina ya
Fuso, namba za usajili T167 AQG.
No comments: