LORI LA MAFUTA LIMEKAMATWA NA JESHI LA POLISI MKOANI IRINGA LIKISAFIRISHA SHEHENA YA VIPODOZI HATARI
Taswira ya nje na Ndani ya lori hilo baada ya kutolewa vipodozi hivyo
mwonekano wa lori kwa nyuma
Jina la kampuni linalomiliki lori hilo
Kamanda wa polisi mkoa wa Iringa ,Ramadhan Mungi akionyesha lori la mafuta lililokuwa na shehena ya vipodozi
Baadhi ya vipodozi vilivyokamatwa
Maofisa wa mamlaka ya chakula na dawa Manispaa ya Iringa wakikagua vipodozi hivyo
Kamanda wa polisi mkoa wa Iringa
Ramadhan Mungi akionyesha shehena ya vipodozi ambavyo vimekamatwa
vikisafirishwa ndani ya lori la mafuta
JESHI la polisi mkoa wa
Iringa limewakamata watu wawili akiwemo dereva wa tenki la
mafuta lenye namba za usajili T 247 BHP wakisafirisha shehena ya
vipodozi maboksi 779 vikiwa vimewekwa ndani ya tenki hilo la mafuta
kutoka nchi za kusini mwa Tanzania kuelekea jijini Dar es Salaam .
Kamanda
wa polisi wa mkoa wa Iringa Ramadhan Mungi alisema kuwa lori
hilo lenye namba za usajili T 247 BHP likiwa na tela lenye namba T
598 BMK ni mali ya kampuni ya World OIL Ltd ya Jijini Dar es Salaam
lilikuwa likiendeshwa na Mohamed Sadru (23) mkazi wa Mbezi Temboni
jijini Dar es Salaam .
Mbali
ya dereva huyo pia jeshi hilo linamshikilia mfanyabiashara
aliyekuwa akisafilisha mzigo huo Bw Kassim Kaifa (23) mkazi wa
jijini Dar es Salaam kwa tuhuma za kuhusika na mzigo huo.
Kamanda
Mungi aliwaeleza wanahabari jana kuwa mtego wa jeshi la polisi
uliweka baada ya kupokea taarifa kutoka kwa rai wema kuhusiana na
lori hilo kutumika isivyo kwa kusafirisha vipodozi hivyo.
Alisema
kuwa taarifa kuhusiana na lori hilo kusafirisha vipodozi badala ya
mafuta waliitapata kutoka jana na mtego wa kulikamata lori
hilo umefanikiwa majira ya saa 9 alfajiri ya jana
Hata
hivyo alisema kuwa sehemu kubwa ya vipodozi hizo ni vile
ambavyo vilipigwa marufuku na serikali kutokana na kuwa na madhara
makubwa kwa afya ya watumiaji wa vipodozi hivyo.
Alisema
kuwa jeshi la polisi limefanikiwa kumata vipodozi hivyo kwa
kushirikiana na mamlaka ya chakula na dawa ,wakala wa barabara
mkoa wa Iringa na mamlaka ya mapato Tanzania (TRA)
Kamanda
huyo alisema kuwa watuhumiwa hao watafikishwa mahakamani mara
baada ya uchunguzi kukamilika na kuwa ni mapema kwa sasa kuitaja
thamani ya vipodozi hivyo na nchi ambayo lori hilo lilikuwa
likitoka kutokana na sababu za kiusalama.
No comments: