Ads Top

WAZIRI WA FEDHA NA UCHUMI DR WILLIAM MGIMWA AMEFARIKI DUNIA KUTOKA NCHINI AFRIKA KUSINI AMBAKO ALIKUWA AKIPATIWA MATIBABU

Waziri wa Fedha, Dk. William Augustao Mgimwa (63) enzi za uhai wake
 Rais Jakaya Kikwete 

Katibu Mkuu Kiongozi Ombeni Sefue 
 Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mheshimiwa Jakaya Mrisho Kikwete amepokea kwa mshtuko na huzuni kubwa taarifa za kifo cha Waziri wa Fedha, Mheshimiwa William Mgimwa, aliyekuwa pia Mbunge wa Jimbo la Kalenga (Mkoa wa Iringa) kupitia Chama cha Mapinduzi (CCM).

Rais Kikwete amesema kuwa taifa limempoteza Waziri Mgimwa katika kipindi lilipokuwa linamhitaji zaidi kutokana na mchango wake mkubwa ambao amekuwa akiutoa kupitia nafasi zake za Waziri wa Serikali na mwakilishi wa wananchi wa Jimbo la Kalenga.

Kifo cha Mheshimiwa Mgimwa kimetangazwa mchana wa leo, Jumatano, Januari Mosi, 2014, na Katibu Mkuu Kiongozi (KMK) Balozi Ombeni Sefue kwa niaba ya Serikali ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania.

Katika tangazo lake, Balozi Sefue amesema kuwa Waziri Mgimwa ameaga dunia asubuhi ya leo saa 5:20 (Saa za Afrika ya Kati) katika Hospitali ya Kloof Medi-Clinic , Pretoria, Afrika Kusini ambako amekuwa amelazwa kwa muda sasa.

Balozi Sefue amesema kuwa maandalizi ya kuurudisha nyumbani mwili wa Waziri Mgimwa yanafanywa na Serikali kwa kushirikiana na familia yake na kuwa taarifa zaidi za suala hilo zitatolewa baadaye kwa kadri zinavyopatikana na maandalizi yanavyoendelea. --
THE UNITED REPUBLIC OF TANZANIA 

DIRECTORATE OF PRESIDENTIAL COMMUNICATIONS
 Rais pia amewatumia rambirambi wananchi wa Jimbo la Kalenga akisema kuwa wamempoteza mwakilishi na mtetezi mahiri wa maslahi yao.

  Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mheshimiwa Jakaya Mrisho Kikwete amepokea kwa mshtuko na huzuni kubwa taarifa za kifo cha Waziri wa Fedha, Mheshimiwa William Mgimwa, aliyekuwa pia Mbunge wa Jimbo la Kalenga (Mkoa wa Iringa) kupitia Chama cha Mapinduzi (CCM).

Rais Kikwete amesema kuwa taifa limempoteza Waziri Mgimwa katika kipindi lilipokuwa linamhitaji zaidi kutokana na mchango wake mkubwa ambao amekuwa akiutoa kupitia nafasi zake za Waziri wa Serikali na mwakilishi wa wananchi wa  Jimbo la Kalenga.

Kifo cha Mheshimiwa Mgimwa kimetangazwa mchana wa leo, Jumatano, Januari Mosi, 2014, na Katibu Mkuu Kiongozi (KMK) Balozi Ombeni Sefue kwa niaba ya Serikali ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania.

Katika tangazo lake, Balozi Sefue amesema kuwa Waziri Mgimwa ameaga dunia asubuhi ya leo saa 5:20 (Saa za Afrika ya Kati) katika Hospitali ya Kloof Medi-Clinic , Pretoria, Afrika Kusini ambako amekuwa amelazwa kwa muda sasa.

Balozi Sefue amesema kuwa maandalizi ya kuurudisha nyumbani mwili wa Waziri Mgimwayanafanywa na Serikali kwa kushirikiana na familia yake na kuwa taarifa zaidi kuhusu suala hilo zitatolewa baadaye kwa kadri zinavyopatikana na maandalizi yanavyoendelea.

Katika salamu zake kwa Waziri Mkuu Mheshimiwa Mizengo Pinda na kwa familia ya Marehemu Mgimwa, Rais Kikwete amesema:  “Sina maneno ya kutosha kuelezea mshtuko na huzuni yangu kubwa kufuatia taarifa za kifo cha Mheshimiwa Mgimwa. Binafsi nimemtembelea mara mbili kwenye Hospitali alikokuwa amelazwa na mara ya mwisho hali yake ilikuwa imeimarika. Tulizungumza kwa kiasi cha dakika 10 hivi akanielezea nia yake na tamaa yake ya kurejea nyumbani kwa sababu hali yake ilikuwa nzuri.”

Ameongeza Mheshimiwa Rais Kikwete: “Sote tunajua mchango wake katika Serikali. Sote tulitamani kuendelea kuwa naye, lakini haya ni mapenzi ya Mungu.”

“Napenda kutoa pole nyingi na rambirambi zangu za dhati kwa wana-familia wote kwa kuondokewa na mhimili wao. Naungana nanyi katika kuomboleza msiba huo mkubwa. Napenda mjue kuwa msiba huu ni msiba wangu pia. Machungu yenu ni majonzi yangu,”
 amesema Rais Kikwete.

Rais pia amewatumia rambirambi wananchi wa Jimbo la Kalenga akisema kuwa wamempoteza mwakilishi na mtetezi mahiri wa maslahi yao.

Imetolewa na:
Kurugenzi ya Mawasiliano ya Rais,
Ikulu,
DAR ES SALAAM.

01 Januari, 2014
----   Wasifu Wa Profesa William Mgimwa
Salutation Honourable
First Name: William
Middle Name: Augustao
Last Name: Mgimwa
Member Type: Constituency Member
Constituent: Kalenga
Political Party: CCM
Member Status: Current Member
Date of Birth 20 January 1950

EDUCATION
School Name/Location Course/Degree/Award Start Date End Date Level
Institute of Development Management, IDM, Mzumbe MBA (Finance) 1989 1991 MASTERS DEGREE
Institute of Finance Management, IFM Postgraduate (Finance) 1983 1984 POSTGRADUATE
Institute of Finance Management, IFM Advanced Diploma (Banking) 1975 1978 ADV DIPLOMA
Tosamaganga Seminary School O-Level Education 1968 1969 SECONDARY
Mafinga Seminary School O-Level Education 1970 1971 SECONDARY
Wasa Primary School Primary Education 1961 1965 PRIMARY
Tosa Seminary Primary School Primary Education 1966 1967 PRIMARY

EMPLOYMENT HISTORY
Company Name Position From To
The Parliament of Tanzania Member - Kalenga Constituency 2010 2015
Bank of Tanzania Training Institute (Mwanza) Principal 2000 2010
The National Bank of Commerce (NBC) - Bank Director 1997 2000
The National Bank of Commerce (NBC) - Bank Manager 1996 1997
The National Bank of Commerce (NBC) - College Lecturer 1981 1989
The National Bank of Commerce (NBC) - Bank Accountant 1980 1981

POLITICAL EXPERIENCE
Ministry/Political Party/Location Position From To
Chama Cha Mapinduzi, CCM Ward Guardian (Wasa, Iringa) 2008 2010
Chama Cha Mapinduzi, CCM Assistant Commander (UVCCM) 1994 1995
Chama Cha Mapinduzi, CCM Councillor (Gangilonga Ward) 1991 1994
PUBLICATIONS

Description
Date
W. Mgimwa: Liquidity Management, Tanzania Bankers Journal, Dar Es Salaam. 1994
W. Mgimwa: Commercial Bank Lending Journal, Dar Es Salaam. 1995
W. Mgimwa: Advanced Credit Operations, Dar Es Salaam. 2007
W. Mgimwa: Advanced Treasury Management, Dar Es Salaam. 2009

No comments:

UHURUTZ. Theme images by hanoded. Powered by Blogger.