Maelfu ya watu wanaendelea kuwasili katika uwanja mkubwa wa FNB mjini Johanessburg kwa kuhudhuria misa ya wafu ya hayati Nelson Mandela
Rais wa Marekani Barack Obama na katibu mkuu wa Umoja wa Mataifa Ban
Ki-moon watakuwa miongoni mwa viongozi wa dunia watakaohudhuria misa
hiyo.
Misa hiyo itafanyika katika uwanja ambako Nelson Mandela alionekana kwa mara ya mwisho hadharani.
Misa hiyo itaonyeshwa kwenye skrini kubwa nje ya uwanja ili kuzuia msongamano wa watu.
Mandela alifariki akiwa na umri wa miaka 95 na kwa wengi yeye ni shujaa na mkombozi wa Afrika Kusini.
No comments: