Msanii wa Muziki wa kizazi kipya Afande Sele Aung'uruma Kata ya Kichangani, jimbo la Morogoro Mjini
Msanii Wa Muziki wa kizazi kipya BongoFleva Selemani
Msindi (Afande Sele)akihutubia Jumamosi hii, mamia ya wananchi wa Kata
ya Kichangani, jimbo la Morogoro Mjini ambao aliwahakikishia wanachi, kama
watashikamana na kusiliza maneno ya busara yanayotolewa na viongozi wa
CHADEMA, basi lazima CHADEMA itachukua madiwani wengi na nafasi ya
ubunge, Jimbo la Morogoro Mjini.
Sehemu ya Umati wa Wananchi na wanachama wa Chadema wakimsikiliza
Msanii wa Muziki wa Kizazi Kipya BongoFleva Selemani
Msindi (Afande Sele) Jumamosi hii, akihutubia mamia ya wananchi wa Kata
ya Kichangani, jimbo la Morogoro Mjini, aliwahakikishia wanachi, kama
watashikamana na kusiliza maneno ya busara yanayotolewa na viongozi wa
CHADEMA, basi lazima CHADEMA itachukua madiwani wengi na nafasi ya
ubunge, Jimbo la Morogoro Mjini.
Alieleza sababu za wanamziki wenye upeo
mkubwa kuingia katika siasa, kwamba wanasiasa wameziba masikio na
hawataki kusikiliza jumbe zao kupitia muziki. Kabla ya kupanda jukwaani
alikanusha kabisa, kushiriki katika kuikosoa kamati kuu ya CHADEMA na
maamuzi yake, kwani yeye anaipenda CHADEMA, Muundo wake, Katiba na vikao
vyake, na hana muda wa kuzungumza mambo yaliyowekwa katika mitandao,
yakimhusisha na kauli zisizo za kweli, eti kwamba analaani uamuzi wa
kamati kuu. Alisema hizo ni njama zinazopangwa kumchonisha na chama
anachokipenda, na kamwe hazitafanikiwa. Kazi imeanza na sasa hakuna
kulala mpaka kieleweke.
No comments: