PONGEZI KWA MAAFISA NA ASKARI WA JESHI LA MAGEREZA WALIOSHIRIKI GWARIDE RASMI LA MAADHIMISHO YA MIAKA 52 YA UHURU
Gadi ya Wanaume ya Jeshi la Magereza ikipita mbele ya Rais wa Jamhuri ya
Muungano wa Tanzania na Amiri Jeshi Mkuu wa Majeshi ya Ulinzi na
Usalama(hayupo pichani)katika mwendo wa haraka kama inavyoonekana katika
picha.
Gadi ya Wanawake ya Jeshi la Magereza ikiwa katika mwendo wa pole kama
wanavyoonekana katika picha wakipita mbele ya Rais wa Jamhuri ya
Muungano wa Tanzania na Amiri Jeshi Mkuu wa Majeshi ya Ulinzi na
Usalama(hayupo pichani).
Kamishna Msaidizi Mwandamizi wa Magereza, Gideon Nkana akitoa hotuba
fupi kwa niaba ya Kamishna Jenerali wa Jeshi la Magereza kwa Washiriki
wa Gwaride rasmi la Maadhimisho ya Miaka 52 ya Uhuru wa
Tanganyika(hawapo pichani). Hafla hiyo fupi imefanyika jana Desemba 09,
2013 katika Ukumbi wa Bwalo Kuu la Maafisa wa Magereza, Ukonga Dar es
Salaam.
Baadhi ya Maafisa na Askari wa Jeshi la Magereza walioshiriki kikamilifu
Gwaride rasmi la Maadhimisho ya miaka 52 ya Uhuru wa Tanganyika
wakisakata rumba mara baada ya kumaliza shughuli ya Paredi. Hafla hiyo
fupi iliandaliwa na Kamishna Jenerali wa Magereza, John Casmir Minja kwa
lengo la kuwapongeza Makamanda hao kutokana na umahiri, ukakamavu
waliouonyesha katika Gwaride la Maadhimisho ambapo hafla hiyo imefanyika
katika Ukumbi w Bwalo Kuu la Maafisa wa Magereza, Ukonga Dar es Salaam.
Baadhi ya Wataalam wa Magwaride wa Jeshi la Magereza wakisikiliza hotuba
ya Mgeni rasmi wakati wa hafla fupi ya kuwapongeza Washiriki wote wa
Gwaride la Maadhimisho ya miaka 52 ya Uhuru wa Tanganyika. Hafla hiyo
fupi iliyoandaliwa na Kamishna Jenerali wa Magereza, John Casmir Minja
kwa lengo la kuwapongeza Makamanda hao imefanyika jana Desemba 09, 2013
katika Ukumbi wa Bwalo Kuu la Maafisa wa Magereza, Ukonga Dar es
Salaam.Picha zote na Jeshi la Magereza
No comments: