Taarifa ya Uchunguzi Juu ya Jaribio la Kuchoma Ofisi Za Chadema Mkoani Arusha
Sehemu inayosemekana waliingia watu waliochoma ofisi
Sehemu ya Ofisi ya Chadema Mkoani arusha iliyochomwa moto
Juzi 3/12/2013 jaribio baya lilifanyika dhidi ya kuchoma ofisi ya CHADEMA ya Kanda ya Kaskazini na Mkoa wa Arusha .
Hata
hivyo Jeshi la Polisi lilifika kwa ajili ya uchunguzi wa awali na Chama
kilielekeza Kitengo chake cha Usalama na Ulinzi kuanza kufuatilia jambo
hilo kwa kina ili kubaini wahalifu wa jaribio hilo baya . Taarifa
ambazo tumepokea mpaka sasa ni taarifa muhimu ambazo tunahamini
zitaisadia Jeshi la Polisi katika uchunguzi wake.
Tumepeleka
majina ya Watu ambao taarifa zetu za kina zinaonyesha wanahusika na
tukio hili takribani wasiozidi watano na ni imani yetu kuwa Jeshi la
Polisi litachukuwa hatua muhimu katika uchunguzi wao huku Chama tukiwa
tiyari kabisa kutoa ushirikiano wa dhati katika uchunguzi wa kina na
wakitaalaamu ambao utaweza kuthibitisha udadisi wetu na uchunguzi wetu
ili kuponya Taifa letu .
Hata hivyo Chadema kinalitaka Jeshi la Polisi kutokufanya Siasa katika jambo hili kwani ni muhimu wakaelewa kwamba kupuuza uchunguzi wa jambo hili ni hatari kwa Mkoa wa Arusha na mustakabali wa Amani ya Taifa letu . Chama katika utafiti wake kimebaini kuwa miongoni mwa washukiwa katika tukio hili wamekuwa ni Vijana ambao wamekuwa wakifanya kazi na Polisi katika jitihada za kuhujumu Chadema na hivyo kunaleta mashaka makubwa juu ya uchunguzi wa jambo hili kama utafanyika kwa ufasaha na weledi wa hali ya juu kwa majina ambayo Chama imemkabidhi Kamanda wa Polisi Mkoa .
Hata
hivyo katika uchunguzi wake Chadema inasikitishwa sana na kitendo cha
Serikali kumpatia mmoja wa washukiwa umiliki wa silaha aina ya bastola
wakati Mtu huyo akiwa na rekodi ya kuwa na kichaa cha mara kwa mara .
Chadema
Kanda ya Kaskazini inawataka Wanachama wake na wafuasi watulie kimya
bila kutafakari aina yeyote ya kisasi kwa jaribu hili baya ili kutoa
fursa njema kwa Viongozi wao na Jeshi la Polisi ili kuwabaini Watu hawa
waliotaka kuteketeza Ofisi ya Chama kwa moto . Lakini pia Chadema
inamshukuru sana na kumpongeza mmiliki wa nyumba hiyo kwa kutambua
majaribu ambayo tumepitia wakati huu kwa kukubali kurekebisha nyumba
ambayo ni ofisi yetu kwa gharama zake mwenyewe kama sehemu ya kuheshimu
jitihada za kushinda hofu na woga unaotaka kupandikizwa miongoni mwa
jamii yetu .
NANYARO E.J.
Mwenyekiti Wilaya
4/12/2013
NANYARO E.J.
Mwenyekiti Wilaya
4/12/2013
No comments: