Watu 12 wamekufa na wengine 44 wamejeruhiwa vibaya baada ya basi la kampuni ya Burdan linalofanya safari zake kutoka wilayani Korogwe kwenda jijini Dar es salam kuacha njia kisha kupinduka.
Basi la Burudani baada ya ajali jana Wilaya ya Handeni, Tanga.
Madaktari na wauguzi wa Hospitali ya Korogwe wakitoa huduma kwa majeruhi.
Madaktari na wauguzi wa Hospitali ya Korogwe wakitoa huduma kwa majeruhi.
DC wa Wilaya ya Korogwe, Mrisho Gambo akiwa Hospitalini hapo kutoa Huduma kwa Majeruhi.
Wananchi wa Korogwe wakiwa nje ya Hospitali hiyo ya Wilaya ya Korogwe.
Taarifa kutoka wilayani Korogwe
ambazo zilithibitishwa na Mkuu wa Wilaya ya Korogwe, Mrisho Gambo
zinasema kuwa watu 12 wamepoteza maisha kufuatia ajali ya basi
la Shukrani.
Basi hilo lililotokea jijini Dar es Salaam kwenda Tanga lilipata ajali eneo la Kabuku kijiji cha Taula Wilaya ya Handeni na
kujeruhi watu wengine 93 kati yao watu 9 wamejeruhiwa vibaya na
kukimbizwa katika Hospitali za KCMC Mjini Moshi na MOI jijini Dar esa
Salaam.
No comments: