WANANCHI WAISHIO UKONGA JIJINI DAR ES SALAAM WAGOMEA FIDIA KIDUCHU YA BOMBA LA GESI
Mwenyekiti wa
Kamati ya kufatilia malalamiko ya wananchi wa mji mpya relini Bw. Omari
Msusa kushoto akihojiwa na vyombo vya habari kuhusu fidia wanayotakiwa
kulipwa huku Mbunge wa Jimbo la Ukonga Dar es Salaam, Bi,Eugen Mwaiposa
akimsikiliza kwa makini
mbunge wa jimbo
la Ukonga Dar es salaam, Bi,Eugen Mwaiposa (kulia) akisikiliza
malalamiko ya wananchi wea eneo la Mji Mpya Relini jimboni kwake jana
wakilalamika kutaka kulipwa fidia ndogo ambazo hazilingani na thamani ya
nyumba zao
Mwenyekiti wa Serikali ya Mtaa wa Mjipya Relini,Ilala Dar es Salaam Bw. Geofrey Chacha (aliyesimama) akitoa malalamiko ya wananchi mbele ya mbunge wa Jimbo la Ukonga, Bi. Eugen Mwaiposa wa pili kushoto wanaolalamikia kuhusu tahmini ya fidia ndogo inayopitishwa ili kupisha upanuzi wa bomba la gesi linalotoka Mtwara. |
Na Mwandishi wetu
WANANCHI
wa Mji mpya Relini wilaya ya Ilala waliopitiwa na mradi ya bomba la
gesi ya Mtwara wamemuomba Mbunge wa Jimbo la Ukonga, Bi. Eugen Mwaiposa
awasilishe bungeni hoja ya kukataa mradi huo kutokana na kupunjwa fidia
ya nyumba na mali zao wanayotakiwa kulipwa.
Bw. Josephat Haule alisema waathirika wenzao katika Kata za Kivule, Pugu Kwalala na Mbande wao wamethaminiwa vizuri na wanatarajia kupata fedha za kujenga nyumba nyingine kutokana na gharama kuwa juu lakini wao nyumba iliyojengwa kwa sh. mil 57 anathaminiwa alipwe sh. mil. 11 na nyumba zenye thamani ya sh. mil. 10 wanataka alipwe sh, mil 3.
"Wananchi wangu wanadhiki, wanashida ya fedha lakini si kwa
malipo kidogo kiasi hicho, tunapiga picha tuoneshe umma thamani ya
nyumba na kiasi wanachotakiwa kulipwa ili wakaendelee na maisha yao
sehemu nyingine" alisema Bi. Mwaiposa.
Bi. Mwaiposa alikiri kuona nyumba zilizothaminiwa kwa fedha kidogo
ambazo haziwezi kununua kiwanja kingine ambavyo kwa sasa katika maeneo
hayo vinauzwa kati ya sh. mil. 10 mpaka sh. mil. 15 kwa kiwanja cha nusu
hekari.
No comments: