DIWANI ATOA AHADI HEWA UJENZI WA ZAHANATI
DIWANI
wa Kata ya Ludete Sebastian Milando ( CCM ) anadaiwa kuwadanganya wapiga kura
wake baada ya kuahidi kuchangia mifuko 25 ya saruji kwa ajili ya ujenzi wa
Zahanati ya Mtaa wa Afya iliyoko katika Mtaa wa Afya Mji mdogo wa Katoro Mkoani
Geita Tanzania Daima limeelezwa.
Wakizungumza
na waandishi wa Habari wananchi wakazi wa Mtaa wa Afya wameeleza kusikitishwa
na vitendo vya mwakilishi wao huyo ambaye ameshindwa kutimiza ahadi hiyo tangu
alipoahidi septemba mwaka jana kwenye mkutano wa hadhara na kwamba diwani huyo
alitoa kali ya mwaka Agosti mwaka huu baada ya kuibuka na kufanya ujenzi wa
choo cha futi tatu katika Zahanati ya Mtaa wa Afya bila kumshirikisha
Mwenyekiti wa Mtaa.
Wakati hayo yakifanyika Mwenyekiti wa Serikali
ya Mtaa wa Afya Masaga Misso alikuwa anashikiliwa
katika gereza la Biharamulo baada ya Viongozi 51 wa Chama cha Demokrasia na
Maendeleo CHADEMA kukamatwa wakiwa katika vikao vya Chama Wilayani Chato ambapo
Viongozi hao walishikiliwa gerezani hapo kwa siku arobaini na tano
Mwenyekiti huyo wa Umoja wa Wenyeviti wa
Serikali za Mitaa Wilaya ya Geita Masaga Misso alikamatwa akiwa na viongozi
wenzake wa CHADEMA Mkoa wa Geita akiwemo Mwnyekiti wa Chama hicho Mkoa Fabian
Mahenge, Mwenyekiti wa Balaza la Wazee Mkoa Vitus Makoye,Mwenyekiti,BAVICHA
Neema Chozaile pamoja na
Hata hivyo baada ya Mwenyekiti huyo kutoka
mahabusu ya Magereza Wilayani Chato alikutana na taarifa za kufanyika kwa
ujenzi wa choo ambacho kinadaiwa kuwa na kina cha futi tatu na kwamba Misso
alipiga marufuku mwendelezo wa ujenzi huo na kuamua kujenga choo cha kisasa kwa
ajili ya kuhakikisha wakina mama katika Mtaa wake wanapata huduma nzuri.
“Mimi nawapenda wananchi wangu,siwezi kufanya
ujenzi wa aina hiyo ni bora Diwani angeacha kufanya siasa katika masuala ya
Afya za wananchi choo cha futi tatu! hivi akina mama wakitumbukia humo ni
hasara ya nani?
Sasa mimi kama kiongozi niliyepewa dhamana ya
kuongoza Mtaa huu nimeamua kujenga choo cha kisasa kitakachogharimu jumla ya
shilingi 1,800,000.”alisema Misso.
Imeelezwa kuwa baada ya kukamatwa kwa
Mwenyekiti huyo na kushikiliwa kwa siku arobaini na tano,Diwani huyo alitangaza
kuwa Mwenyekiti huyo amefungwa na hatatoka gerezani hivyo alianza kampeni ya
kupanga safu kwa ajili ya kufanyika kwa uchaguzi marudio na chanzo cha ujenzi
wa choo hicho feki.
Mwenyekiti huyo wa Serikali ya Mtaa wa Afya ambaye pia ni
Mwenyekiti wa Umoja wa Wenyeviti wa Serikali za Mitaa Wilaya ya Geita Masaga
Misso, ameanza ujenzi wa choo cha kisasa pamoja na kukarabati majengo mawili ya
Zahanati hiyo ambapo ujenzi huo
unatarajia kukamilika mapema septemba mwaka huu na kwamba ujenzi wa Choo hicho utagharimu
kiasi cha shilingi mil 1,800,000 huku ukarabati wa majengo ya Zahanati
ukigharimu kiasi cha shilingi mil 36 .
Tanzania Daima lilimtafuta Diwani wa kata ya
Ludete Sebastian Milando kuzungumzia
tuhuma na malalamiko hayo ambapo alikana na kusema yeye hajui jambo lolote kati
ya hayo yanayozungumzwa dhidi yake
“Mimi sijui chochote wacha waseme”alijibu Milando na kukata simu.
MWISHO
No comments: