AGIZO LA JPM LASIMAMISHA SHUGHULI ZA KIJAMII KWA SAA MBILI
Na
Antony Sollo Sumbawanga.
AGIZO la Rais wa Jamhuri ya Muungano wa
Tanzania John Pombe Magufuli la kufanya siku ya Jumamosi ya mwisho wa mwezi
kuwa siku ya usafi wa mazingira le oleo limeleta simanzi na majionzi kwa
wananchi wa Manispaa ya Sumbawanga na vitongoji vyake Tanzania Daima linaweza
kuripoti.
Wakizungumza na Tanzania Daima wananchi
waliokuwa wamekaa makundi katika mitaa mbalimbali wakisubiri tamko la
Mkurugenzi wa Manispa ya Sumbawanga ili wafungue biashara zao wananchi hao
wamelaani kitendo cha Ofisi ya Mkurugenzi kuwapa adhabu ya kufungua kinyume na
tamko la Rais Magufuli ilivyozoeleka kwao ambapo kwa kawaida wamekuwa
wakifungua saa nne baada ya kumaliza shuguli za usafi wa mazingira.
Awali Mkuu wa Mkoa wa Rukwa Zelothe
Steven akiongozana na viongozi mbalimbali wa Manispaa ya Sumbawanga alipita
katika maeneo mbalimbali kukagua zoezi la usafi wa mazingira ambapo msara huo
ulianzia soko kuu na kuhitimisha katika soko la sabasaba.
Akiwa katika soko la sabasaba Mkuu huyo
wa Mkoa alisikitishwa na hali ya soko hilo lilivyokuwa chafu na kuamuru
viongozi wa Manispaa hiyo kusimamia vizuri majukumu yao na kuwataka watimize
wajibu wao.
“ Nawaombeni kila mmoja atomize wajibu
wake maana tukiwa tunasubiri siku iliyotamkwa na mh Rais tutakuwa hatujui
vizuri wajibu wetu hivyo basi naomba kuwaambia ukweli kuanzia sasa mtumishi
yeyote atakayezembea kutimiza wajibu wake hatutamvumilia”.alisema Zelothe.
Baada ya kukamilika kwa shughuli za
usafi katika soko la sabasaba,Mkuu wa Mkoa aliwataka wananchi kuzingatia usafi
ili kuzilinda Afya za wananchi.
“Ndugu zangu wananchi,naomba muelewe
kuwa usafi siyo jambo la kupuuzwa maana Afya zetu ni muhimu kuliko kitu
chochote hivyo jengeni tabia ya kufanya usafi bila kushurutishwa”alisema.
Kuhusu kucheleweshwa kufungua biashara
kwa zaidi ya saa mbili wananchi wameilalamikia Serikali kutokana na uharibifu
ambao umetokea kufuatia kuharibika kwa bidhaa zao zikiwemo nyanya,supu na
samaki wabichi na kuiomba Serikali kuondoa mkanganyiko wa maelekezo ambapo
kulikuwa na madai kuwa Mkurugenzi wa Manispa hiyo alitoa kauli tata kuwa
wafanyabiashara wasifungue biashara zao mpaka hapo yeye atakapopenda jambo
lililopingwa vikali na wananchi hao.
Mmoja wa wananchi hao Yusuf Masunga
ameulalamikia uongozi wa Manispaa ya Sumbawanga kwa kushindwa kuheshimu sheria
na kuziomba mamlaka zinazohusika kuwathamini wafanyabiashara maana ndiyo chanzo
cha mapato ya Halmashauri ya Manispaa hiyo.
“Sisi wafanyabiashara ni wadau muhimu wa
maendeleo ya Manispaa ya Sumbawanga,tunalipa ushuru,kodi, na mambo mengine sasa
kitendo cha kutuzuia kufungua biashara zetu ni kukiuka maadili na haki maana
iwapo tabia hii haitakemewa itafika mahala mtu mmoja atafikia uamzi wa kuamuru
wananchi wakalale na wataamka atakapopenda yeye”alisema Mayunga.
Tanzania Daima lilimtafuta Mkurugenzi wa
Manispaa ya Sumbawanga Hamid Njovu ili kujibu tuhuma zilizotolewa kuhusu kauli
ya kutofunguliwa kwa biashara mpaka yeye atakapopenda ambapo Mkurugenzi huyo
aliruka futi miamoja kwa kuelekeza swali hilo aulizwe Mkuu wa Mkoa wa Rukwa
Zelothe Steven ambapo hata hivyo Mkuu huyo wa Mkoa alisema kwamba hatuwezi
kufanya shughuli za biashara bila kuzingatia usafi wa mazingira.
No comments: