WATANZANIA WAISHIO KENYA WAITIKIA WITO WA KUJITOLEA DAMU KWA AJILI YA WAATHIRIKA WA TUKIO LA UGAIDI, NAIROBI KENYA,BALOZI WA TANZANIA NCHINI KENYA BATILDA BURIANI AWA MFANO

 
Mh. Balozi Batilda S. Burian akiwa katika zoezi la kutolewa damu pamoja na watanzania wengine aliyoambatana nao.

Balozi
 wa Tanzania nchini Kenya Mhe Batilda S. Burian,  leo ameongoza umati wa
 Watanzania waishio hapa Nairobi, Kenya,  kujitolea damu kwa ajili ya 
kuwasaidia waathirika wa tukio la ugaidi lililotokea Tarehe 21 Septemba 
2013 jijini Nairobi Kenya, ambapo   hadi sasa zaidi ya watu 62 
wamepoteza maisha na wengine zaidi ya 179 wamejeruhiwa vibaya na wengi 
wao bado wanaendelea kupata matibabu katika hospitali za Aga Khan 
University Hospital, Hospitali ya Nairobi ( Nairobi Hospital), na 
Hospitali ya MP Shah.Picha Kwa hisani ya Issa Michuzi 
Katika
 tukio hilo pia Mtanzania, Bwana Vedastus Nsanzungwanko, Meneja, Child 
Protection, UNICEF ni mmoja wa wale walioathirika na tukio hilo ambapo 
alijeruhiwa  kwa risasi na magruneti katika miguu yake yote miwili. Hivi
 sasa Bwana Vedastus amelazwa katika hospitali ya Aga Khan, Nairobi na 
anendelea kupatiwa matibabu na hali yake inaendelea vizuri.
No comments: